Majaliwa aridhishwa na mradi mkubwa wa umeme..


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi II ambao ukikamilika utazalisha jumla ya megawati 240 zitakazoingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo uliopo  eneo la Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Amesema baada ya kukagua amejionea kazi nzuri inayoendelea katika ujenzi wa mradi huo unao tekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Sumitomo ya Japan.
"Mradi huu ni wa kimakakati kwa ajili ya kuzalisha umeme ili Watanzania wapate nishati hii kwa bei nafuu. Ndiyo Maana Serikali imeamua kuanzisha uhusiano na balozi tofauti kwa ajiki ya kutekeleza miradi mbalimbali," amesema Majaliwa.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakisha nishati ya umeme inafika vijijini kupitia mradi unaotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambao umeonekana kufanya vizuri katika maeneo mengi nchini.
Alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuendelea kusambaza umeme kwa wananchi wengi.


Source:Mwananchi 





















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..