Akamatwa kwa kummulika kwa mionzi rubani wa helikopta ya polisi..

Helikopta ya Polisi iliyokuwa doria angani katika mkutano wa G20 iliyolengwa kwa mionzi ili kumpofusha macho rubani wake


Polisi nchini Ujerumani imesema inamshikilia mtu mmoja anayetuhumiwa kutaka kusababisha mauaji baada ya kutumia kifaa cha mionzi kummulika rubani wa helkopta  ya polisi iliyokuwa ikifanya doria angani wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za kundi la G20 mjini hamburg.
Mshukiwa huyo anadaiwa alilenga kuleta upofu wa macho wa muda kwa rubani huyo ili asababishe ajali.
Katika taarifa ya Polisi iliyotolewa leo, Jumamosi Kijana huyo wenye miaka  27, ambaye jina lake halikutajwa kutoka na Sheria ya faragha ya Ujerumani alifanikiwa kuwatia upofu wafanyakazi wawili katika helkopta hiyo wakati wakiwa angani na kupelekea kusimamisha kazi zao kwa sababu ya kutoona.
Tukio hilo lilitokea Alhamisi ya juma hili.
Kufuatia uchunguzi wa kina, polisi walifanikiwa kumkamata mshukiwa huyo katika nyumba yake huko Hamburg leo, Jumamosi pamoja na kumkuta na kifaa hicho cha mionzi.
Maelfu ya wanaharakati wanaopinga utandawazi wamekuwa wakipamba na polisi kwa siku mbili mfululizo huku viongozi hao wa G20 wakiendelea na mkutano wao.




Source:Azamtv
























































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..