MTU MMOJA ATIWA MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 11...
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mwanaume mmoja Makusudi Rashidi (39) kwa kudaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 11 jambo lililomsababishia maumivu makali sehemu za siri.
Imeelezwa kuwa mwanaume huyo mkazi wa mtaa wa Ibangaja wilayani Ilemela Jijini Mwanza alifanya kosa hilo wakati watoto hao wakiwa wamelala nyumbani na wazazi wao ghafla aliingia chumbani na kumuingilia kwa nguvu kimwili mtoto huyo ndipo mtoto huyo alipoanza kupiga kelele huku akiomba msaada baada ya mtuhumiwa kuona hali hiyo ametoka nje na kuanza kukimbia.
Wakizungumzia tukio hilo kwa masikitikito baadhi ya wananchi wamesema kuwa hali hiyo ni ya kinyama na kuliomba Jeshi la Polisi kumchukulia hatua kali za kisheria mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha kutokea tukio hilo lakini pia kutoa wito kwa wazazi na walezi akiwaomba kuwa na makazi salama yatakayoweza kuwalinda watoto dhidi matukio hayo.
Source:Modewjiblog
Maoni
Chapisha Maoni