Nafasi 3 za wachezaji ambao walipata thamani kubwa ya soko wakati wanastaafu soka...
Kuna wachezaji hawawezi kuchoka miili yao hata kama ametangaza kustaafu kucheza soka, ni kawaida kwa wchezaji wanapofikia kuzeeka kisoka na hata pia soko lao upungua zaidi. Kuna baadhi ya wachezaji wamestaafu na ujuzi wao ulikuwa bado upo uwanjani.
Na hii ndio list ya wachezaji 3 wenye thamani kubwa sokoni kipindi walichokuwa wanastaafu kucheza mpira.
1.ZINEDINE ZIDANE
Zinedine Zidane alikuwa moja ya wachezaji bora katika kipindi chake cha uchezaji mpira, pia anajumuishwa kama ni moja wa kiungo bora zaidi duniani aliyewahi kutokea katika kipindi chake cha soka. Na bado jina lake linazungumzwa mpaka sasa, ukizungumzia wachezaji nyota waliowahi kutokea jina lake lazima litokee.
Alistaafu soka kipindi akiwa na umri wa miaka 34, Zidane alikuwa na thamani ya Pauni 10.63 Millioni, wishoni mwa kipindi chake cha uchezaji, mwaka 2016.
2.PHILIPP LAHM
Mchezaji huyu wa kijerumani aliyekuwa anacheza nafasi ya nyuma (Beki), ni mchezaji ambaye alichezea timu yake ya Taifa Ujerumani na pia Klabu ya Bayern Munich, pia alijulikana kwa uchezaji wake wa kujituma katika pande zote mbili za timu ya Taifa na Klabu. Lahm amestaafu mwishoni mwa msimu huu uliopita (Mei 2017), na thamani yake ilikuwa Pauni 9.35 Millioni.
3.WILLY SAGNOL
Willy Sagnol anajumuishwa kama ni miongoni mwa beki bora wa upande wa kulia katika kipindi chake cha uchezaji mpira.Baada ya kusajiliwa na Bayern Munich mwaka 2000, haikumhukuwa muda mrefu kukaa na Klabu yake ya mwanzo.Wakati akiwa na Klabu ya Bavarian alishinda ligi ya Bundesliga mwaka 2001,2003,2005,2006 na 2008. Alistaafu soka akiwa bado ana umri mdogo 31, na thamani yake ilikuwa Pauni 8.08 Millioni, kipindi cha mwaka 2009.
Maoni
Chapisha Maoni