Pigo kwa Venezuela: Marekani yawawekea vikwazo maafisa 13..

Askari wa Venezuela wakipambana na waandamanaji


Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo maafisa 13 wa vyeo vya juu wa Venezuela wakati mashinikizo yakizidi kuongezeka dhidi ya Rais Nicolas Maduro kabla ya kura inayokumbwa na utata ya bunge jipya la kuandika katiba mpya.
Walengwa wa vikwazo hivyo miongoni mwao ni waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa majeshi.
Wiki iliyopita, Rais Donald Trump aliapa "kuchukua hatua ngumu na kubadili uchumi wa nchi hiyo"  iwapo Maduro hataruhusu uchaguzi, uliopangwa kufanyika Jumapili.
"Hawa mabepari wa Marekani wanafikiri wao ni kina nani?" alisema Maduro Jana, Jumatano. "Serikali ya dunia?"
Na pia ameviita vikwazo hivyo "haramu, kinyume na  visivyokubalika".



Source:AzamTv


















































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..