Al Jazeera yakosoa Israel kutaka kufunga ofisi zake Jerusalem...

Ofisi za runinga ya Al Jazeera mjini Doha, Qatar

Runinga ya Al Jazeera imekosoa vikali kitisho cha waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu cha kutaka kufungwa kwa ofisi ya runinga hiyo mjini Jerusalem.
Aljazeera imejibu tuhuma za Netanyahu alizoziandika kwenye facebook akisema runinga hiyo inachochea vurugu.
Pia Netanyahu aliandika kuwa atatunga sheria ya kuiondoa Aljazeera nchini kwake Israel, endapo tafsiri za sasa za kisheria zitashindwa kutoa nafasi ya kufungwa kwa runinga hiyo.
“Matamshi ya Netanyahu ni muendelezo wa matukio yenye nia mbaya dhidi ya Al Jazeera,” inasema taarifa ya Al Jazeera ikirejea wito wa baadhi ya nchi za Ghuba zikiongozwa na Saudi Arabia ambazo hivi karibuni zilitoa wito wa kufungwa kwa runinga hiyo.
"Al Jazeera inasisitiza kuwa itachukua hatua zote stahiki za kisheria kama kitisho cha Israel kitakuwa halisi,” iliendelea kusema taarifa hiyo ya Aljazeera.
Aljazeera imesema kuwa itaendelea kuandika habari za eneo la Palestina kwa uweledi na bila upendeleo.
Na matamshi hayo ya Netanyahu yamekuja huku kukiwa na mgogoro katika mji wa Jerusalem ambako serikali yake ilikuwa imefunga vifaa maalumu vya usalama kuwachunguza Wapalestina wanaokwenda kuswali kwenye msikiti wa al-Aqswa.
Kwa muda mrefu, Netanyahu amekuwa akiilalamikia Al Jazeera juu ya uandikaji wake wa habari za eneo la Palestina, ambalo limekuwa na vurugu nyingi kufuatia hatua ya Israel kuendelea kukalia baadhi ya makazi ya Wapalestina.


Source:AzamTv

































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..