Wanaocheleweshwa safari za ndege 'kulamba mamilioni'..

Hamza Johari akiwa katika mazungumzo na wanahabari


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga nchini Tanzania (TCAA), Hamza Johari amewataka watuamiaji wa huduma za anga nchini kutambua haki zao pindi yanapotokea mapungufu ya kizembe wakati wa matumizi ya vyombo vya usafiri wa anga nchini.
Amesema kwa mujibu wa sheria na taratibu, watoa huduma wa sekta ya anga wanapaswa kuwajibika iwapo litatokea tatizo la kizembe kama vile abiria kuchelewesha au kupotelewa na mizigo au hata ajali ya kizembe.
Hamza amesema kwa abiria anayecheleweshwa anapaswa kulipwa dola za Marekani 6000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 13 za kitanzania, wakati abiria anayepotelewa na mizigo atalipwa dola 1500 sawa na shilingi milioni 4 za kitanzania.
“Iwapo mtumiaji wa huduma ya usafiri wa anga atapata tatizo la kuchelewa kwa ndege anatakiwa alipwe dola 6000, kama kutakuwa na upotevu wa mizigo, mtoa huduma atalipa dola 1500 na kama ni ajali mtoa huduma ya usafiri wa anga anatakiwa kulipa dola 120,000 na kuendelea". Amesisitiza Mkurugenzi huyo wa Mkuu TCAA
Amesema iwapo kutatokea tatizo la aina hiyo, mtumiaji wa huduma ya usafiri wa anga anapaswa kutoa taarifa za kimaandishi kwa shirika husika, baraza la watumiaji, na kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ili taratibu za faini zieweze kuendelea
Pia Hamza amewahakikishia watanzania kuwa mamlaka hiyo imejipanga kuboresha sekta ya usafiri wa anga katika kuelekea uchumi wa kati huku akiipongeza serikali kwa kulirejesha kwa kasi Shirika ya Ndege Tanzania (ATCL).



Source:Azamtv

































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..