Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2015

Mpira utakaotumiwa kwenye ligi ya England msimu ujao.

Picha
Kukiwa kumesalia mizi miwili na siku kadhaa kabla ya ligi kuu ya England na lingi nyingine kubwa barani ulaya kuanza mpira rasmi utakaotumika kwenye ligi ya England umefahamika . Mpira huo umebuniwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Kimarekani ya Nike ambapo utakuwa unafahamika kwa jina la Nike Ordem na umetengenezwa kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa ambayo inaendana na mabadiliko ya mchezo wa soka . Mpira huo umetengenezwa kwa kuzingatia jinsi ambavyo wachezaji watakuwa wakiutumia uwanjani ambapo moja ya vitu vilivyozingatiwa ni rangi yake na umetengenezwa kwa rangi angavu ili kuwasaidia wachezaji kuuona wakiwa uwanjani na kufanya maamuzi ya haraka. Beki wa West Ham United James Tomkins akiwa anaujaribu mpira mpya ambao utatumika kwenye msimu ujao wa ligi ya England . Mpira huo pia una sehemu 12 ambazo zinaufunika ili kuusaidia kwenda na kasi ambayo itawasaidia wachezaji wenye uwezo wa kupiga mashuti ya mbali . Mpira huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa mwezi julai p...

Picha tatu za Boti ya KILIMANJARO V ilivyoshushwa kwenye maji Zanzibar

Picha
Usafiri wa Boti ndio kiungo muhimu cha Dar na Zanzibar, watu wengi wanautegemea usafiri huu mtu wangu.. Good news kwa wasafiri wote DAR-ZANZIBAR !! Boti nyingine tayari imeshushwa kwenye maji Zanzibar na time yoyote itaanza safari kati ya Dar na Zanzibar, ninazo pichaz zikionesha Boti hiyo ilivyoshushwa toka Australia. Source; (Millard Ayo.com)

Uchina kuweka kambi ya kijeshi Djibouti.

Picha
Kambi ya wanajeshi wa Marekani iliyoko Djibouti Djibouti, nchi ndogo iliyoko kwenye mwambao wa bahari ya shamu tayari inahifadhi vituo vya kijeshi vya Marekani na Ufaransa, mtawala wake wa zamani wa kikoloni. Lakini ari ya Uchina ya kutaka kuweka kituo chake cha kijeshi nchini Djibouti sasa imebainika wazi. Swali ni je, ni nini hasa kinachovutia katika nchi hii ya pembe mwafrika na kulengwa na mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi duniani? Udhabiti wa kisiasa wa Djibouti katika eneo lenye mizozo mingi ni kigezo kikubwa. Viongozi wa Djibouti na Somalia Djibouti iko kwenye mwambao wa Bab el-Mandeb, lango la kuingia mfereji wa Suez, ambao ni mojawapo wa njia za meli yenye shughuli nyingi zaidi duniani. Lakini kuwepo kwa Djibouti karibu na maeneo mengine ya Afrika na Mashariki ya Kati kunaifanya nchi hiyo iwe kivutio kikubwa cha mataifa yenye uwezo mkubwa wa kisiasa kuweka vituo vyao vya kijeshi. Kusini Magharibi kuna Somalia ambayo imezongwa na mzozo wa ...

Balozi Seif atembelea uwanja wa Mao Tse Tung.

Picha
Mhandisi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Ali Mbarouk (katikati) akimuonyesha Balozi Seif, ramani ya uwanja wa Mao Tse Tung utakavyokuwa baada ya kukamilika. MATAYARISHO ya ujenzi wa kiwanja cha michezo cha Mao Tse Tung, Mjini Zanzibar, yameanza rasmi kwa hatua ya utafiti wa udongo wa eneo hilo. Mhandisi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Ali Mbarouk alieleza hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara fupi ya kukagua matayarisho hayo. Mhandisi huyo alimueleza Balozi Seif kwamba, utafiti huo wa udongo unafanywa kwa kuchukuwa aina tofauti za udongo kwenye vishimo 34 kwenye eneo la uwanja. Utafiti huo unatarajiwa kuchukuwa muda wa siku 20. Alisema udongo huo utafanyiwa utafiti wa kina na wataalamu waliobobea na baadaye watatoa ripoti kamili itakayofuatiwa na utangazaji wa tenda kwa makampuni yatayokuwa tayari kujenga uwanja huo. Alifahamisha kazi ya ujenzi ya uwanja huo inatara...

Wabunge wahamasishwa kununua hati fungani.

Picha
Spika wa Bunge, Anna Makinda. Spika wa Bunge, Anna Makinda GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu amewahamasisha wabunge kununua hati fungani zinazotolewa na Benki Kuu kama njia ya kuhifadhia fedha zao na kupata faida. Gavana Ndulu alitoa hamasa hiyo jana wakati akijibu hoja za wabunge, wakati wa semina iliyotolewa na BoT juu ya mwenendo wa thamani ya shilingi ya Tanzania mjini Dodoma. Alisema mpaka sasa ni Watanzania wachache wanaonufaika na hati hizo, na baadhi yao ni wageni kutoka nje. “Wageni wanatazama, wananunua hati hizi fungani ama vipande vinavyouzwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja (UTTAMIS),” alisema. Aliwashauri wabunge watakapolipwa mafao yao baada ya Bunge kumalizika wiki chache zijazo, wachangamkie fursa hizo za uwekezaji kwa kuwa una faida. Alisema mtu anayewekeza pesa zake kwenye hati hizo, hasubiri hadi uwekezaji kuiva, miaka mitano au saba, bali kila baada ya miezi sita anapokea fedha. Alisema mtu anayewekeza kwenye hati hizo ana uhaki...

Pinda aunga foleni ya wasaka urais.

Picha
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionesha mkoba wenye fomu ya kuwania kuteuliwa na CCM kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu baada ya kuchukua fomu hiyo, Dodoma jana. Kulia ni mkewe, Tunu Pinda na Katibu wa Oganaizesheni wa NEC, Mohamed Seif Khatib. (Picha na Ofisi Waziri Mkuu) WAZIRI Mkuu jana amejitosa rasmi kuchukua fomu na kuingia katika kinyang’anyiro cha kuomba kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015. Pinda, ambaye amekuwa mgombea wa 32 kuomba fursa hiyo ndani ya CCM amesema Mungu pekee ndiye anayemjua mwanachama atakayeteuliwa kugombea nafasi hiyo, huku akitamani Mungu ampe kibali cha kuongoza Watanzania kwani ana lengo la kuwafikia wanyonge. Pinda alifika Makao Makuu ya CCM saa nne asubuhi akiwa ameambatana na mkewe, Tunu Pinda, huku baadhi ya wabunge wakimsindikiza katika kumuunga mkono kwenye hatua yake ya kuwania nafasi hiyo. Akizungumza mara baada ya kuchukuwa fomu, Pinda alisema endapo atapata nafasi ya kushika nafasi hiyo ya juu nchi...

Shilingi kurejea kawaida yake.

Picha
Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania Prof BENNO NDULU alipokuwa Akitoa Ufafanuzi Juu Ya Ubora Wa Noti Mpya (Picha na Maktaba). BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha thamani ya Shilingi ya Tanzania, hatua ambazo imesema katika kipindi kifupi kijacho zitaifanya sarafu hiyo kuimarika. Kasi ya kushuka kwa thamani ya Shilingi imekuwa kubwa ambapo takwimu za wiki hii zinaonesha kwamba Dola ya Marekani ilikuwa inabadilishwa kwa wastani wa zaidi ya Sh 2,000 za Tanzania kutoka Sh 1,629 Machi 2014. Akiwasilisha mada kuhusu mwenendo wa thamani ya Shilingi katika semina liyoandaliwa na BoT kwa ajili ya wabunge mjini Dodoma jana, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, alitaja moja ya hatua zilizochukuliwa kuwa ni kuongeza mauzo ya Dola katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (IFEM). Soko hilo la jumla (Interbank Foreign Exchange Market- IFEM) ndilo ambalo kwa sehemu kubwa linatoa mwelekeo wa kiwango cha ubadilishanaji wa fedha za kigeni. Hatua nyingine a...

Watu 141 wakamatwa katika msako.

Picha
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu JESHI la Polisi nchini kupitia Kitengo cha Interpol limewakamata watu 141 kwa makosa mbalimbali kupitia operesheni maalumu iliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 4 hadi 5, mwaka huu ikiwa imefanyika kwa wakati mmoja katika nchi 25 wanachama barani Afrika. Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Diwani Athumani alisema wamekamata jumla ya watuhumiwa 141 katika operesheni iliyopewa jina la operesheni II inayohusisha makosa mbalimbali. “Taarifa hii inatokana na operesheni tuliyoifanya kwa makubaliano ya Kanda za Polisi ya Interpol kuwa iwepo kwa nchi 25 kutoka Kanda ya Kusini mwa Afrika (Sarpocco) na Kanda ya Afrika Mashariki (EAPCCO) na pia imefanyika kwa siku mbili katika tarehe hiyo kwa nchi zote wanachama,” alisema Athumani. Alisema walifikia makubaliano hayo ya kuwa na operesheni maalumu itakayofanyika kwa wakati mmoja ili kuweza kukabiliana na matukio mbalimbali ya kih...

Serikali kuendelea kutafiti Nishati mbadala.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma yake ya kukamilisha Mradi wa Utafiti wa Nishati mbadala ili kujuwa uwezekano wa Zanzibar kupata Umeme wake wa uhakika. Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla  Shaaban katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  Chukwani  wakati akitoa Hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2015 /2016. Amesema Wizara yake imekamilisha kazi ya kupatikana  kwa Mkandarasi  kutoka katika Kampuni ya (AGMIN ya Italy )kwa Ujenzi wa Minara ambapo kwa sasa ameanza kazi zake. Aidha amefahamisha kuwa Mshauri Elekezaji wa ukusanyaji wa taarifa pamoja na kutayarisha Ripoti ya upembuzi  sahihi ( Feasibility Study) ameshapatikana ambapo kazi yao inatarajiwa kumalizika Mwaka ( 2017) Itakumbukwa kuwa Zanzibar bado inategemea Nishati ya Umeme kutoka Tanzania Bara na kwamba kama Utafiti huo utatoa Matokeo mazuri kuna uwezekano wa Zanzibar kuwa na Vyanzio vyake...

Interpol yakata ushirikiano na FIFA.

Picha
Polisi wa kimataifa wavunja uhusiano wao na FIFA Shirika la polisi wa kimataifa Interpol limesema linasimamisha uhusiano wake na FIFA uliokuwa na lengo la kuchunguza na kukabiliana na visa vya upangwaji wa matokeo ya mechi za kandanda, kutokana na kashfa ya rushwa inayolizonga shirikisho hilo la soka duniani. Miaka minne iliyopita FIFA iliipa interpol dolla millioni 22 kufadhili mradi ulio na lengo la kuendeleza maadili katika secta ya michezo. Interpol inasema washirika wake wote ni sharti wadumishe na kuendeleze maadili na taratibu zinazotumiwa na interpol katika utendaji kazi wake. FIFA imesema imesikitishwa na uamuzi huo wa Interpol na kuongeza kuwa mradi huo wa mikakati ya kuzua udandanyifu katika soka hauhusiani kwa vyovyote vile na kashfa ya madai ya rushwa dhidi ya FIFA. Source(BBC SWAHILI).

Afrika yatakiwa kutotegema misaada.

Picha
Ujumbe wa Twitter wa rais Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema wakati umefika kwa mataifa ya Afrika kukoma kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje. Kwenye ujumbe alioutuma katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, rais Kenyatta amesema misaada hiyo ya kigeni mara nyingi huwa na vikwazo na masharti ambayo yanakandamiza. Ameongeza kusema kuwa hatma ya bara la afrika siku zijazo haipaswi kuwa mikononi mwa mataifa ya magharibi ambayo mara nyingi huweka maslahi yao kwanza. Kenya hutegemea mabilioni ya dola kila mwaka yanayotolewa na mataifa ya kigeni na katika bajeti ya mwaka wa 2015-16 waziri wa fedha wa Kenya alijumuisha misaada kutoka nje katika makisio ya serikali ya mwaka huu. Source(BBC SWAHILI).

Vyama 17 kususia uchaguzi Burundi.

Picha
Burundi Kundi moja la vyama 17 nchini Burundi limekubaliana kususia uchaguzi mkuu wa mwezi ujao likisema kuwa hautakuwa huru na haki. Upinzani unasema kuwa rais Pierre Nkurunziza hafai kuwania muhula wa tatu. Pia wanataka uchaguzi huo kuahirishwa ,msimamo unaoungwa mkono na viongozi wa eneo hili. Taifa la Burundi limekumbwa na maandamano na majaribio ya mapinduzi yaliofeli tangu rais Pierre Nkurunziza kutangaza mwezi Aprili kwamba atawania muhula mwengine. Source(BBC SWAHILI)

Baraza la famasia lakiri kutokusajili kozi ya famasia inayotolewa na chuo cha KIU.

Picha
Baraza la famasia nchini limesema halijasajili kozi ya famasia inayotolewa na chuo kikuu cha Kampala kampasi ya Dar es Salaam kwa sababu hakijakidhi matakwa ya kusajiliwa huku uongozi wa chuo hicho ukizungumzia suala hilo. Msajili wa baraza hilo Bi Zainabu Kamingoma ameyasema hayo katika mahojiano maalum na ITV ambapo amedai kuwa uongozi wa chuo hicho ulikosea tangu awali baada ya kujenga majengo na kuanza kusajili wanafunzi bila ya kushirikisha baraza wala kuomba usajili na kwamba majengo na vifaa siyo kigezo cha wao kupata usajili.   Kufuatia maelezo hayo ITV imeutafuta uongozi wa chuo cha Kampala ili kuzungumzia sakata hilo ambapo naibu mkurugenzi wa udahili wa chuo hicho Bw Lotha Samora mbali na kueleza kushangazwa na kauli ya msajili ameonyesha nyaraka mbalimbali walizopewa na baraza hilo zikiwaruhusu kuendelea kutoa taaluma hiyo na kuhusu wahitimu ambao vyeti vyao havitambuliki wamekubaliana na serikali wavipeleke TCU vikashughulikiwe.   Kwa upande wa wanafu...

Orodha ya nchi 10 zaidi duniani zenye idadi kubwa ya watu kuliko nchi nyingine (2000-2015) na Nigeria ikiwa ndio nchi ya pekee kutoka bara la Afrika

NCHI 10 ZENYE IDADI KUWA YA WATU DUNIANI. # Country 2000 Population 2010 Population 2015 Population 2050 Expected Pop. 1 China 1,268,853,362 1,330,141,295 1,361,512,535 1,303,723,332 2 India 1,004,124,224 1,173,108,018 1,251,695,584 1,656,553,632 3 United States 282,338,631 310,232,863 321,362,789 439,010,253 4 Indonesia 213,829,469 242,968,342 255,993,674 313,020,847 5 Brazil 176,319,621 201,103,330 204,259,812 260,692,493 6 Pakistan 146,404,914 184,404,791 199,085,847 276,428,758 7 Nigeria 123,178,818 152,217,341 181,562,056 264,262,405 8 Bangladesh 130,406,594 156,118,464 168,957,745 233,587,279 9 Russia 146,709,971 139,390,205 142,423,773 109,187,353 10 Japan 126,729,223 126,804,433 126,919,659 93,673,826 TOP TEN Countries 3,618,894,827 4,016,489,082 4,213,773,474 4,950,140,178 Rest of the World 2,466,012,769 2,829,120,878 3,050,850,319 4,306,202,522 TOTAL World Population 6,...

Al Shabaab ladai kuwaua askari wa Ethiopia.

Picha
Al shabaab Kumekua na mapigano makali katikati mwa Somalia baina ya wanajeshi wa taifa hilo ,wanamgambo wa kiislam wa Alshaabab na wanajeshi wa Ethiopia Al Shabaab linasema limewauwa askari 30 wa Ethiopia ambao ni sehemu ya kikosi cha muungano wa Afrika na kuharibu magari saba ya kijeshi . Watu katika kijiji cha Jame kilichopo karibu na mji wa Bur Hakaba wanasema kuwa walisikia milio ya risasi. Hakuna ripoti yoyote kutoka kwa serikali ya Ethiopia kufikia sasa. Kundi la alshabaab limefurushwa katika miji mingi ya Somalia lakini bado linadhibiti maeneo mengi ya mashambani. Source(BBC SWAHILI)

Walimu wakataa kurudi kazini

Picha
Shambuliz la Garissa Walimu ambao walilitoroka eneo la kazkazini mashariki mwa Kenya wakihofia mashambulizi kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Al shabaab wamekataa kurudi eneo hilo. Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay alielezea katika kipindi cha Newsday kwamba asilimia 60 ya walimu hawatoki katika eneo hilo na waliokwenda likizo wengi wamekataa kurudi. Ameelezea kuwa takriban walimu 2000 wamelitoroka eneo hilo na kwamba nusu ya idadi ya shule za eneo hilo zimefungwa. Amesema kuwa wafanyikazi wa uma pia wamelitoroka eneo hilo. Source(Bbc Swahili)

Hong Kong yatoa tahadhari ya MERS.

Picha
Hospitali inayotibu MERS Korea Kusini Serikali ya Hong Kong imetoa tahadhari dhidi ya kusafiri kwenda nchini Korea Kusini, kufuatia kuwepo mlipuko wa homa ya Middle East Respiratory Syndrome ambayo pia inafahamika kama MERS nchini humo. Onyo hilo linatolewa kwa safari ambazo si za lazima, ishara kuwa Hong Kong inaamini kwamba usafiri kwenda Korea kusini ni jambo ambalo ni hatari. Wizara ya afya nchini Korea Kusini inasema kuwa watu 7 kwa sasa wameaga dunia kutokana ugonjwa huo. Kumeripotiwa visa 8 vipya vya homa ya MERS na kufikisha idadi ya watu walioambukizwa kuwa 95. Source(Bbc swahili)