Uchina kuweka kambi ya kijeshi Djibouti.


Kambi ya wanajeshi wa Marekani iliyoko Djibouti
Djibouti, nchi ndogo iliyoko kwenye mwambao wa bahari ya shamu tayari inahifadhi vituo vya kijeshi vya Marekani na Ufaransa, mtawala wake wa zamani wa kikoloni.
Lakini ari ya Uchina ya kutaka kuweka kituo chake cha kijeshi nchini Djibouti sasa imebainika wazi.
Swali ni je, ni nini hasa kinachovutia katika nchi hii ya pembe mwafrika na kulengwa na mataifa yenye uwezo mkubwa wa kijeshi duniani?
Udhabiti wa kisiasa wa Djibouti katika eneo lenye mizozo mingi ni kigezo kikubwa.
null








Viongozi wa Djibouti na Somalia
Djibouti iko kwenye mwambao wa Bab el-Mandeb, lango la kuingia mfereji wa Suez, ambao ni mojawapo wa njia za meli yenye shughuli nyingi zaidi duniani.
Lakini kuwepo kwa Djibouti karibu na maeneo mengine ya Afrika na Mashariki ya Kati kunaifanya nchi hiyo iwe kivutio kikubwa cha mataifa yenye uwezo mkubwa wa kisiasa kuweka vituo vyao vya kijeshi.
Kusini Magharibi kuna Somalia ambayo imezongwa na mzozo wa muda mrefu ambao unaathari za kimataifa kuhusu swala la mabaharia na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al shabaab linalotishia usalama katika kanda ya Afrika.
Yemen, ambayo kwa sasa inakumbwa na misukosuko, iko takribani umbali wa maili 20 tu kutoka Kaskazini Mashariki mwa njia ya Bab-el-Mandeb- ambayo ni kivukio cha haraka cha kuingia Mashariki ya kati.
null








Ufaransa na marekani tayari zinakambi zao za majeshi nchini Djibouti
Mizozo hii kwa pamoja imesababisha jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na haja ya kuweka kambi za kijeshi nchini Djibouti.
Rais Omar Guelleh wa Dibouti hivi majuzi aliambia shirika la habari la AFP kwamba mazungumzo yanaendelea kati ya taifa lake na Beijing ya uwezekano wa Uchina kuanzisha kituo rasmi cha cha jeshi la wanamaji.
Beijing haijakana wala kukubali ripoti hizi ingawa uhusiano huu haujapenedelewa na Marekani, ambayo inawasiwasi kwamba huenda maslahi yake yakahatarishwa na ongezeko la shughuli za kijeshi za Uchina katika eneo hilo.
Source(BBC SWAHILI)












Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..