Bavicha yataka wananchi wasidanganyike wachague viongozi waadilifu.



Baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema limewataka wananchi wasidanganyike na viongozi wanaotumia nguvu kupata madaraka badala yake wapime viongozi waadilifu na wazalendo kwa taifa waliotayari kubadilisha maisha ya watanzania walio wengi na si kujinufaisha wenyewe.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa ifakara wilayani kilombero katibu mkuu wa baraza la vijana wa Chadema taifa Julius Mwita amewataka wananchi kujiandikisha katiba daftari la wapiga kura ili watumie fursa kwenye sanduku la kura kuchagua viongozi wazalendo na si viongozi wenye nia ya kujinufaisha.
 
Naye katibu mwenezi wa baraza hilo Edward Simbeye amesema inashangaza kuona vigogo wanatumia gharama kubwa kutangaza nia ya kugombea urais huku wananchi wakikosa huduma za afya ambapo amewashauri wakazi wa Ifakara kufanya uamuzi mgumu kwa kuchagua viongozi wa Ukawa mwezi Oktoba mwaka huu watakaosaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.
Source(ITV)











Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..