WAFUGAJI NCHINI WAMETAKIWA KUFUATA SHERIA NA KUACHA TABIA YA KUCHUKUA SHERIA MKONONI.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Mohammed Gharib Bilal amewataka wafugaji nchini kuhakikisha wanafuata sheria na kuachana na tabia ya kuchukua sheria mkononi ili kufanikisha usalama wao na watu wengine.
Mheshimiwa BILAL ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa Chama cha Wafugaji Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wao ALLY HAMIS LUMIYE.
Awali akizungumza kwa niaba ya Baraza la Wazee wa Chama hicho Tanzania, Mwenyekiti wa Chama amesema kuwa chama chao kinakabiliwa na changamoto kubwa hususani kuwepo kwa mgawanyiko wa wanachama huku akiiomba serikali kuingilia kati suala hilo ili kuletea maelewano ndani ya chama.
Source(Efm radio)
Maoni
Chapisha Maoni