Jeshi la Polisi Arusha lakamata gunia 124 za Bangi,lita 450 za Gongo na magari 2 ya wizi.
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limekamata gunia mia moja na ishirini na nne za dawa za kulenya aina ya bangi lita mia nne na hamisini za pombe ya gongo na magari mawili yanayo sadikiwa kuwa ni ya wizi huku mtu mmoja akijeruhiwa kwa risasi baada ya kupambana na askari polisi akizuia kunyany’anywa banki anayo miliki.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema operesheni hiyo imefanyika katika vijiji vya Kisimiri juu na Ngaramtoni wilayani Arusha kufuatia taarifa za kuendelea kwa kasi ya uzalishaji wa dawa za kulevya zikiwemo bangi na mirungi ambayo inamadhara makubwa kwa afya za binadamu lakini baadhi ya wakulima wa dawa hizo wameonekana kuwa jeuri na kutaka kupambana na askari.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa vijiji vya Ngaramtoni na Kisimiri waliyozungumza na ITV wamesema wakazi wa vijiji hivyo wameshindwa kuacha kulima bangi kwakuwa hawana uwezo wa kulima zao lingine kutokana na kukosa pembejeo za ruzuku.
Nawo baadhi ya wananchi wanaokerwa na kuenea kwa dawa za kulevya zinazo onekana kuathiri zaidi vijana wamelamikia uzembe wa viongozi wa serikali za vijiji vinavyo endelea na kilimo hicho kuwa wanahusika ndiyo sababu wana endelea kufumbia macho kilimo hicho.
Source(ITV)
Maoni
Chapisha Maoni