Utata kwenye mkataba wa beki wa Liverpool .
Beki wa klabu ya Liverpool Martin Skrtel amefichua kuwa bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo kama ambavyo inaripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini England pamoja na nyumbani kwao huko Slovakia .
Skrtel ambaye kimsingi ni moja kati ya wachezaji muhimu wa klbu ya Liverpool amekuwa kwenye mazungumzo ya muda sasa na klabu yake ambapo ripoti kadhaa zimekuwa zikidai kuwa anakaribia kusaini mkataba mpya .
Akitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Skrtel amesema kuwa ofa ya mkataba ambayo Liverpool imemuwekea mezani haikubaliki kwake na hajasaini kwani haijakidhi mahitaji yake .
iverpool imemthibitisha James Milner kama mchezaji wake mpya .
krtel amedai kuwa Liverpool imempa aina ya mkataba ambao hupewa kwa wachezaji wenye umri mkubwa na wale wenye kuandamwa na majeraha na si mchezaji mwneye mchango kwenye timu kama yeye .
Klabu ya Liverpool kwa siku za hivi karibuni imekuwa kwenye mazungumzo na wachezaji kadhaa juu ya mikataba ambapo mchezaji mwingine Raheem Sterling amekuwa akigoma kusaini mkataba mpya huku ikivumishwa kuwa atahama kwenda klabu ya Man City hivi karibuni .
Taarifa hii inakuja dakika chache baada ya Liverpool kuthibitisha usajili wa kiungo raia wa England James Milner ambaye amesajili akitokea klabu ya Manchester City .
Source(Millardayo.com)
Maoni
Chapisha Maoni