Mbeya City yajitutumua
STRAIKA wa Stand United raia wa Nigeria, Abasalim Chidiebele anakaribia kujiunga na Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili. Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi alisema Mnigeria huyo anatarajiwa kuziba nafasi ya Deus Kaseke na Peter Mwalyanzi ambao wiki iliyopita waliachana na timu hiyo na kujiunga na Simba na Yanga. “Ni mshambuliaji mzuri ambaye naamini kama tutampata ataziba vizuri pengo la Kaseke na Mwalyanzi, ana uwezo wa kumiliki mpira lakini pia ana nguvu kitu ambacho tunakihitaji ili kuwa na safu kali ya ushambuliaji.” Alisema mipango yao ni kupata wachezaji bora wenye uwezo ili kuweza kufikia malengo yao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu, ambayo.
Source(Sports starehe)
Maoni
Chapisha Maoni