VIONGOZI WALIOTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WATAJWA KUSHINDWA KUBAINISHA MIKAKATI YA UTU NA NGUVU YA MWANAMKE



LICHA ya baadhi ya Viongozi wa siasa nchini kutangaza nia za kutaka kugombea nafasi ya urais kupitia vyama vyao, Viongozi hao hawajaweza kubainisha  mikakati ya kuwezesha utu  na nguvu ya mwanamke wa Tanzania kama sehemu muhimu ya mipango yao.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa wanawake na katiba MARRY RUSIMBI wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna watangaza nia wanavyopaswa kupambanua kiundani na changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake wakitanzania.
Naye Mwenyekiti wa mtandao wa wanawake na katiba Profesa RUTH MEENA  amebainisha kuwa ni vyema kwa wanawake waliopo ndani ya vyama kusimama kwa pamoja na kupigania haki zao kwani kwa kufanya hivyo kutachangia kuwepo kwa ushiriki wa wanawake unaoleta tija katika ngazi  za uongozi nchini.
Na kwa upande wake  Mwakilishi kutoka katika Shirika la Wanawake katika Jitihada za kimaendeleo-WAJIKA,  JANETH MAWINZA ameeleza kuwa kama wanawake wameanza kupata hofu kwani watangazania wote waliopita wameshindwa kugusia masuala mazima ya unyanyasaji wa kijinsia kama vile rushwa ya ngono na ubakaki kwa watoto wa kike.
Source(Efm radio)








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..