Kofi Annan amtaka Nkurunziza kujiuzulu


Koffi Annan
Aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan amemtaka rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kujiuzulu huku uchaguzi mkuu ukiahirishwa.
Kumekuwa na maandamano ya ghasia nchini Burundi pamoja na mapinduzi yaliofeli tangu Nkurunziza atangaze kuwa atawania muhula mwengine wa tatu wa urais katika kile watu wanaamni ni ukiukaji wa katiba.
Annan ameiambia BBC kwamba rais huyo amepoteza uhalali wake na sasa anafaa kujiuzulu iwapo anawajali raia wa Burundi.








Maandamano nchini Burundi
Matamshi hayo ya Annan yataongeza shinikizo kwa rais Nkurunziza ,ambaye hadi sasa hajatoa ishara zozote za kujiuzulu.
Uchaguzi wa bunge pamoja na ule wa urais umehairishwa kufuatia wiki za maandamano ya ghasia.
Viongozi wa jumuia ya Afrika Mashariki walipendekeza uchaguzi wa bunge na urais uahirishwe kwa wiki sita kufuatia ghasia za kumpinga rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.








Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Uchaguzi wa Rais unatarajiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni.
Source(Bbc swahili)
























Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..