Serikali kuendelea kutafiti Nishati mbadala.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma yake ya kukamilisha Mradi wa Utafiti wa Nishati mbadala ili kujuwa uwezekano wa Zanzibar kupata Umeme wake wa uhakika.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla  Shaaban katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  Chukwani  wakati akitoa Hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2015 /2016.

Amesema Wizara yake imekamilisha kazi ya kupatikana  kwa Mkandarasi  kutoka katika Kampuni ya (AGMIN ya Italy )kwa Ujenzi wa Minara ambapo kwa sasa ameanza kazi zake.

Aidha amefahamisha kuwa Mshauri Elekezaji wa ukusanyaji wa taarifa pamoja na kutayarisha Ripoti ya upembuzi  sahihi ( Feasibility Study) ameshapatikana ambapo kazi yao inatarajiwa kumalizika Mwaka ( 2017)

Itakumbukwa kuwa Zanzibar bado inategemea Nishati ya Umeme kutoka Tanzania Bara na kwamba kama Utafiti huo utatoa Matokeo mazuri kuna uwezekano wa Zanzibar kuwa na Vyanzio vyake vya Umeme badala ya kutegemea Bara.

Waziri Shabani amesema katika utekelezaji huo Wizara imeweza kushiriki katika mikutano mbalimbali iliyofanyika ndani na nje ya Nchi ikiwemo kuhudhuria katika mkutano wa kuitangaza Tanzania katika utekelezaji wa masuala ya Nishati (Den Hague-Uholanzi).


Akielezea kuhusu utekelezaji huo amesema  kuwa ni kushiriki katika Maonesho na Warsha ya Nishati Mbadala iliyo fanyika Kahama na Tanzania, na kushiriki Vikao vya Jumuia ya Afrika Mashariki katika masuala ya Nishati na Umeme (Nairobi Entebe) sambamba na mkutano mkuu wa Mafuta na Gesi wa Afrika Mashariki (EAPCE 2015) uliofanyika Kigali –Ruwanda.

Hata hivyo amesema katika kuhakikisha Nishati ya Mafuta inapatikana Nchini Wizara inaendelea kufuatilia shughuli za kusimamia upatikanaji wa Mafuta pamoja na utekelezwaji wa Ratiba za uagizaji wa Mafuta Nchini kwa Makampuni manne makubwa (GAPCO,UP,ZP na PUMA).

Aidha  amefahamisha kuwa katika kulisimamia suala hilo dosari za uagizwaji wa Mafuta ya Petrol zimejitokeza baina ya Mwezi wa Februari na Machi ambazo zilichangiwa na kuchelewa kwa Meli ya Mafuta ya pamoja (Bulk Consignment) inayoleta Mafuta Nchini Tanzania.

Sambamba  na hayo Waziri Shaaban amesema kutokana na hali iliyojitokeza ni kiashirio tosha cha kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Taasisi maalum ya kushuhulikia Sekta Binafsi ya kuendesha Biashara hiyo kwa kutumia sheria.

Waziri Shaaban ameliomba Baraza la Wawakilishi limuidhinishie Jumla ya Shl. Bilion 35 na Milioni 949 kwa ajili ya Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati kwa mwaka wa Fedha 2015-16.  
Source(Zanzi News)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..