Rekodi ya kipekee ya mchezaji Andres Iniesta wa Barcelona.
Unapozungumzia ubora wa mchezaji si wengi wanaweza kubishana na ukweli kwamba Andres Iniesta ni moja kati ya viungo bora kwneye soka la kimataifa na ameweza kubakia katika ubora na kiwango cha juu kwa muda mrefu bila kushuka.
Kiungo huyu amekuwa sehemu ya mafasikio ya klabu hii ya Kihispania kwa muda mrefu tangu alipoanza kucheza akiwa amepandishwa toka kwenye timu za vijana za klabu hii ambayo imekuwa ikisifika kwa kuamini na kutengeneza vijana wake yenyewe.
Iniesta ametwaa mataji yote yaliyoko kwenye soka la ushindani kuanzia ligi ya Hispania , Kombe la Mfalme , Super Coppa Espana, European Super Cup , kombe la dunia kwa vilabu , Kombe la dunia la FIFA pamoja na michuano ya kombe la mataifa ya ulaya .
Kiungo Andres Iniesta ndio mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwenye fainali za mashindano makubwa matatu tofauti.
Akiwa sehemu ya kizazi cha pekee kwneye historia ya soka la Hispania Iniesta ameweza kudumu wakati wachezaji wengi wamekuja na kupita na cha kushangaza ni jinsi ambavyo ameendelea kuwa bora .
Jumamosi ya wiki hii iliyopita , Andres Iniesta aliweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi yaani Man Of The Match kwenye fainali za Ligi ya mabingwa , kombe la Ulaya na kombe la dunia baada ya kutwaa tuzo ya Man Of The Match kwenye fainali dhidi ya Juventus .
Iniesta anakuwa mchezaji pekee ambaye amewahi kuweka rekodi hiyo akiwa katika ubora wake ule ule ambao amezoeleka kuwa nao .
Iniesta alikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa Barcelona dhidi ya Juventus baada ya kutoa pasi ya mwisho iliyosaidia bao la kwanza lililofungwa na Ivan Rakitic kwenye dakika ya 4 na kwenye mchezo wote akiwa kama nahodha kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Xavi Hernandez.
Source(Millardayo.com)
Maoni
Chapisha Maoni