Mabalozi wataka tatizo kupungua kwa Tembo litangazwe kama janga la taifa.



abalozi kutoka nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wamesema tatizo la kuendelea kupungua kwa idadi ya tembo na kupotea kwa tembo zaidi ya elfu kumi katika mfumo wa ikolojia ya hifadhi ya taifa ya ruaha na pori la akiba la Rungwa ni janga la kitaifa linalohitaji nguvu ya pamoja kukabiliana nalo.
Wakiongea kufuatia matokeo ya sensa ya tembo wa Tanzania ya mwaka 2014 ambao idadi yao imepungua na kufikia tembo elfu 43, na tukio la kupotea kwa tembo elfu kumi katika kipindi cha mwaka mmoja ambao hata mizoga au masalia yao hayajaonekana mabalozi hao wakiwemo wa Marekani, umoja wa Ulaya, balozi wa China na balozi wa Ujerumani wamesema kwa kutambua umuhimu wa tembo kwa uhifadhi na maendeleo ya taifa, watakuwa tayari kushikiana na serikali ya Tanzania kuongeza vifaa na kuimarisha ulinzi wa maliasili wakiwemo wanyamapori na hasa tembo ili waendelee kuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.
 
Hivi karibuni waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alitangaza matokeo ya sensa ya tembo iliyofanyika kwenye maeneo tisa ya uhifadhi nchini, chini ya uratibu wa taasisi ya utafiti wa wanyamapori nchini. Tawiri na akaeleza kushangazwa na taarifa za kupotea kwa tembo zaidi ya elfu kumi katika mazingira ya kutatanisha lakini akazungumzia mipango na juhudi mpya katika kuimarisha uhifadhi na kuhakikisha idadi ya tembo inaongezeka na kufikia zaidi ya tembo laki moja miaka 15 ijayo.
 
Waziri Nyalandu pia alizindua kituo cha kulelea watoto yatima wa tembo mjini Arusha ambao watahifadhiwa hapo na baadae kurejeshwa kwenye makazi yao ya asili na pia alizindua helkopita maalum zitakazotumika kwa doria na kupambana na matukio ya ujangili kwenye maeneo mbalimbali ya uhifadhi nchini, miradi itakayotekelezwa na serikali ya Tanzania  kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi wa ndani na nje ya nchi.
Source(ITV)



















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..