Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2015

Tume ya Uchaguzi Tanzania yasema iko tayari..

Picha
Jaji Damian Lubuva. Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imekutana na wamiliki wa vyombo vya habari Jumatano na kuwapa muhtasari wa maandalizi ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu Katika mkutano huo mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva ameeleza kwamba kwa kiasi kikubwa maandalizi ya uchaguzi mkuu yamekamilika ambapo sasa wako katika mchakato wa mwisho wa kuchapisha daftari la wapiga kura baada ya kuweka hadharani lile la awali huku vifaa vingine vya uchaguzi vikiwa vimekamilika kwa asilimia kubwa. Naye Kaimu mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi Emmanuel Kawishe aliwahakikishia wamiliki wa vyombo vya habari juu ya kuwepo na umakini wa kutosha katika uhakiki wa kura mara baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika Tume ya taifa ya uchaguzi pia ilizungumzia kuahirishwa kwa chaguzi mbili za ubunge katika majimbo mawili ambayo baadhi ya vyama vimepoteza wagombea wao kwa kufariki dunia, katika majimbo ya Lushoto kwa CHADEMA na Ulanga m

Taswira You Tube:Itizame Video Inayoonesha Vyuo 10 bora Duniani (2015), Ikiwa Afrika hakuna hata Kimoja...

Picha

KAMPENI ZA MAGUFULI ZATUA UWANJA WA JAMHURI DODOMA...

Picha
Mgombea urais wa  Tanzania  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John pombe Magufuli leo akiwa katika Mkoa wa  Dodoma  ambao ni wa 18 kufanya kampeni zake, amefanya mikutano katika vijiji na majimbo mbalimbali. miongoni mwa vijiji hivyo ni Mbande, Chunyu, Mpwapwa, Kongwa, Kibaigwa, Chalinze, Njia Panda ya Chamwino na kumalizia na mkutano ulihudhuliwa na maelfu ya wananchi katika uwanja wa Jamhuri mjini  Dodoma. Magufuli akiendelea kujinadi kwa wakazi wa Mkoa wa  Dodoma  jioni ya leo. Msanii maarufu wa Bongo fleva, Ally Saleh Kiba 'King Kiba' akitoa burudani kwa wakazi wa  Dodoma  wakati wa mkutano huo. Msanii maarufu wa Bongo fleva, Khaleed Ramadhan Tunda 'Tunda Man' naye akifanya yake Chege na Temba wakikamua jukwaani. SOURCE:Muungwana Blog

EU yatuma kikosi cha waangalizi 140 wa uchaguzi..

Picha
Umoja wa Ulaya (EU) umetuma kikosi cha watu takriban 140 watakaofanya uangalizi wa mwenendo wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika siku 23 zijazo.  Waangalizi hao wanaojumuisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya uchaguzi, wanasiasa, baadhi ya maofisa kutoka balozi za nchi za EU nchini, na waangalizi waliajiriwa kutoka  Tanzania , watakuwemo nchini hadi mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.  Mkuu wa kikosi cha uangalizi cha EU, (EU EOM), Judith Sargentin amewaambia wanahabari leo kuwa kikosi hicho kitakuwa na kazi kuu ya kuangalia iwapo uchaguzi utafanyika kwa kufuata misingi, sheria na kanuni za nchi, za kikanda na zile za kimataifa  kama  misingi ya kujenga demokrasia.  Amesema tayari baadhi ya waangalizi walishaanza kuwasili nchini mwanzoni mwa Septemba ikiwemo timu ya wataalamu wa masuala ya siasa, uchaguzi na sheria zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi iliyowasili nchini Septemba 11.  “Katika kipindi chote cha uangalizi tutakuwa huru, hatutafungamana na upand

Dk Shein akelwa na wapinzani kupotosha ukweli wa hoja ya suala la mafuta na gesi visiwani...

Picha
Mgombea urais wa serikali ya mapinduzi Zanziba kupitia chama cha mapinduzi CCM Dk. Aly Mohamed Shein amelalamikia wapinzani wake kwa kupotosha ukweli wa hoja ya suala la mafuta na gesi visiwani humo akidai kukamilisha mswaada wake na baraza la wawakilishi mapema mara baada a uchaguzi mkuu. Akihutubia katika viwanja vya Paje kusini Unguja katika mfululizo wa kampein zake za kuwania kiti cha urais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar awamu ya saba Dk. Aly Mohamed Shein amewahakikishia wazanzibari kuwa mswaada huo pamoja na sera ya mafuta na gesi vinalenga kuwanufaisha wazanzibari na taifa lao kiuchumi na kijamii.   Katika kuelezea kile alichokiainisha kuwa ni upotosha ji wa mahasibu wake katika majukwaa ya kampei kuwa hadi sasa hakuna kilichofanyika kuhusu suala la mafuta na gesi kwa mstakabali wa Zanziba na kuitumia kama turufu ya kujiombea kura wakikandamiza upande wa pili hali alioielezea kuwa haimtendei haki na kuwataka wazanzibari kupuuza upotoshwaji huo. SOURCE:ITV

Mtoto wa Marehemu Paul Walker kapeleka Kesi ya Kifo cha baba yake Mahakamani, madai yake ni haya….

Picha
Marehemu  Paul Walker   alikuwa mmoja ya wakali ambao wamecheza movie za  Fast & Furious … Kifo chake ni moja kati ya vifo vilivyoshtua na kuwaumiza watu wengi Duniani. Jamaa alifariki kwa ajali ya gari aina ya   Porsche Carrera GT  ambayo ilikuwa inaendeshwa na rafiki yake,  Roger Rodas  na  Paul   mwenyewe alikuwa amekaa upande wa pili.. hiyo ilikuwa November 30 2013, California Marekani. Hili ndio eneo ambalo  Paul Walker  alipata ajali . Leo kuna story ambayo imepewa uzito sana mitandaoni, inahusu ishu ya mtoto wa kike wa  Paul Walker   ambaye anaitwa  Meadow Rain Walker  mwenye umri wa miaka 16… amefungua mashtaka kuishtaki Kampuni ya  Porsche  kwamba ajali iliyopelekea kifo cha baba yake miaka miwili iliyopita, ilitokana na gari kuwa na matatizo na anadai kwamba muundo wa gari hiyo haikuwa gari ya kutembelea, ila ilikuwa na muundo wa gari ya mashindano. Kingine ambacho kiko kwenye Mashtaka hayo ni kwamba wanadai gari hiyo haikuwa na mfumo mzuri wa umeme, kwa hi

Tanzania yaongoza duniani kutoa huduma za kifedha kwa simu..

Picha
Dar es Salaam.  Tanzania ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma za pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa kutumia mawasiliano ya simu, kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB) Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inanukuu taarifa ya  Benki ya Dunia  kuwa Tanzania ni moja ya nchi zenye masoko makubwa zaidi duniani ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu. Katika taarifa inaongeza kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiwango cha juu katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ikilinganishwa na nchi nyingine duniani. Kwa mujibu wa Mchumi Mkuu wa WB, Benki Kuu, Prof Kaushik Basu Kenya inaongoza kwa kutuma pesa kupitia mfumo wa M-Pesa katika eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa eneo la kujidai la nchi tajiri tu duniani. “Tuko katikati ya mapinduzi makubwa ya teknolojia, ambayo athari zake bado ni ngumu sana hata kubashiri. Na hizi ni shughuli ambazo miaka michache iliyopita zilikuwa hata hazina jina, lakini sasa inteneti na teknolojia

Kenya: walimu waendelea na mgomo licha ya amri ya mahakama..

Picha
Shule ya msingi ya Kogelo, magharibi mwa mji wa Nairobi, moja ya shule zinazokabiliwa na mgomo wa walimu. Mgomo wa walimu umeendelea nchini Kenya, huku shule nyingi zikifungwa licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu warejee shuleni Jumatatu wiki hii. Mgomo huu wa walimu nchini Kenya umeingia wiki yake ya tano.Vyama vya walimu vimeapa kutotekeleza amri ya mahakama iliyowataka kusitisha mgomo kwa siku tisini kuanzia Jumatatu wiki hii. Hata hivyo vyama hivyo vya walimu vimeripoti mahakamani kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi wa Mahakama wa kuwataka walimu kurejea shuleni. Lakini kesi hiyo imeahirishwa hadi Alhamisi Octoba 1, 2015. Walimu walijitokeza kwa wingi wakiandamana na viongozi wao wa vyama vya walimu walipojielekeza mahakamani.Walimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha mgomo uliposhika kasi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi alhamisi saa nane u nusu kwa sababu jaji aliyekuwa akisikiza kesi hiyo aliomba

Makamu wa rais Dk Bilal amewaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Mh.Kombani jijin DSM...

Picha
Makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal amewaongoza waombolezaji kuuaga mwili wa aliyekuwa waziri wa nchi, ofisi ya rais, menejimenti ya utumishi wa umma Mh Celine Kombani zoezi lililofanyika viwanja vya Kareemje jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Morogoro kwa maziko. Mara baada ya mwili huo kuwasili katika viwanja hivyo mchungaji Wilfred Mmari ameongoza ibada fupi ya kumuombea marehemu kabla ya makundi mbalimbali kutoa salaam zao za rambirambi.   Akisoma salamu za serikali waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama mbali na kueleza uadilifu uliotukuka wa marehemu Kombani amesema ndani ya serikali ameacha pengo huku mwakilishi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar naye akitoa salaam.   Naye spika wa bunge anayemaliza muda wake Mh Anne Makinda akitoa salaam kwa niaba ya ofisi ya bunge amewataka watumishi wa umma kutumia msiba huo kutafakari na kurekebisha maisha yao kwa kuwa na upendo na kuwatumikia wananchi kwa kutoa hu

ITAZAME TRAILER YA MOVIE YA CRISTIANO RONALDO INAYOTOKA MWEZI WA 11

Picha

STURRIDGE JUU ZAIDI YA TORRES NA SUAREZ LIVERPOOL..

Picha
Mshambuliaji Daniel Sturridge wa Liverpool ameweka rekodi ya kuwa na wastani mzuri wa kufunga katika ligi kuu England ndani ya klabu ya Liverpool baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Aston Villa weekend ya jana. Sturridge ameifungia Liverpool magoli 37 katika mechi 57 alizoichezea klabu yake kati ya michezo ya ligi kuu ya England na kuweka wastani wa kufunga goli 0.65 kwa mechi na kuipita ile ya Fernando Torres wa 0.64. Pamoja na majeruhi ya mara kwa mara, Sturridge amefunga magoli 42 kati ya michezo 69 aliyoichezea Liverpool katika mashindano mbalimbali. Luis Suarez aliifungia Liverpool magoli 69 kati ya michezo 110 akiwa na wastani wa kufunga goli 0.63 Michael Owen alifunga magoli 118 kati ya michezo 216 aliyoichezea klabu hiyo huku akiwa na wastani wa kufunga goli 0.55 kwa mechi. Daniel Sturridge ana nafasi kubwa ya kuongeza wastani huo kwa kuwa bado ana muda mrefu zaidi wa kucheza klabuni hapo. SOURCE:Shaffihdauda.com

Wasanii wa Bongo movie waibukia Iringa watangaza kutembea nchi nzima kwa Bajaj kumuunga mkono Dkt Magufuli...(PICHAZ)

Picha
Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-IRINGA.  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa. Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kweny