Mh.Lowassa ahidi kuinua uchumi wa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kujenga viwanda...



Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Mh.Edward Lowassa amewaahidi kuinua uchumi wa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuanzisha viwanda vitakavyozalisha ajira na kuinua kipato cha wakazi hao.

Katika siku yake ya kwanza ya kampeni mkoani Lindi akitokea mkoani Mtwara, huku akitumia usafiri wa chopa, Mh.Edward Lowassa amefanikiwa kunadi ilani ya UKAWA kila kona ya mkoa wa Lindi huku akihutubia mikutano mikubwa katika majimbo ya Mtama, Liwale, Nachingwea, kabla ya kuhitimisha katika jimbo la Lindi mjini ambapo ameahidi kufungua mikoa hiyo ya kusini kwa kuifanya kuwa mikoa yenye viwanda vingi zaidi kutokana na rasilima nyingi zilizoko ndani ya mikoa hiyo.
 
 Fredirick Sumaye waziri mkuu mstaafu amewataka wakazi hao na watanzania kwa ujumla kuendelea kuwapuuza wale wote wanao walaghai wanaowatisha watanzania kwa kuwambia kuwa wasithubu kuchagua upinzani kwani kwa kufanya hivyo ni kuiingiza nchi katika machafuko.
 
Mh.Edward Lowassa na timu yake ya kampeni inatarajiwa kuanza kunadi ilani yake ya uchaguzi kwenye majimbo ya Kiteto, Babati, Simanjiro na Merelani mkoani Manyara.






SOURCE:ITV













Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..