Mbeya City yaapia kwa Azam...


Mbeya MBEYA City imeondoka jijini Mbeya na kutamba inakuja kufuta rekodi zake zote mbovu ndani ya Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam pale itakapokwaana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Kesho. 

Akiizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alisema kikosi kizima cha timu yake kipo salama Dar es Salaam kwa lengo la kusaka ushindi tu.

 Kimbe alisema, kuanza vibaya kwa ligi si kwamba ndiyo wamefeli bali ni mwanzo tu lakini kesho wana uhakika mkubwa wa kuichapa Azam. “Mara nyingi kuanza vibaya siyo kwamba ndo umefeli nasema ule ulikuwa mwanzo tu lakini kesho tuna uhakika wa kuchukua pointi zote tatu mbele ya Azam pamoja na ukweli kuwa kila tukicheza pale tunapata sare ila tunafuta hiyo,” alisema.

 Alisema, lengo ni kuvunja mwiko katika uwanja huo, kwani msimu uliopita kati ya mechi nne walizocheza hapo, walipata sare tatu na kushinda moja. Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Matawi ya Mbeya City, Thimothy Mwalongo, alisema mashabiki kadhaa wa timu hiyo waliondoka jana usiku kwa ajili ya kwenda kuipa sapoti. “Kama unavyojua tupo kila mahali pamoja na timu yetu, hatujawahi kuiacha, tunakwenda Chamanzi kwa lengo moja tu la kuisapoti timu, misimu miwili iliyopita tuliweka rekodi ya kuujaza uwanja huo, nina uhakika haijawahi kuvunjwa na tunataka kuivunja wenyewe msimu huu.”



SOURCE:Sports Starehe




















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..