Raia wafagia mji mkuu Burkina Faso..

Burkina Faso
Utamaduni wa kufagia barabara za miji ulianza wakati wa uongozi wa Thomas Sankara

Raia mjini Ouagadougou, Burkina Faso leo wamekuwa wakifagia mji huo baada ya wiki ya maandamano yaliyosababishwa na mapinduzi ya serikali.
Kaimu Rais Michel Kafando alirejeshwa rasmi mamlakani jana baada ya viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi kuingilia kati na kushawishi waliokuwa wamepindua serikali kung’atuka.
Mwandishi wa BBC katika mji huo mkuu Charlotte Attwood anasema raia hao walisema wamefurahishwa na kurejeshwa mamlakani kwa serikali ya kiraia, na sasa wanataka kusafisha mji.
Wakati wa maandamano, walikuwa wameweka vizuizi barabarani na kuchoma tairi kulalamika dhidi ya walinzi wa rais waliokuwa wamechukua mamlaka.
Mwandishi wa habari wa BBC Africa Lamine Konkobo, anayetoka Burkina Faso, anasema utamaduni wa kufagia barabara za miji, ujulikanao kama ‘operesheni manamana’, ulianza wakati wa utawala wa Thomas Sankara, raia aliyeuawa wakati wa mapinduzi ya serikali 1987.
Kiongozi huyo alikuwa akiwalazimisha wakazi kufagia barabara za miji kila wikendi.
Kwa kufagia mji baada ya maandamano, waandamanaji hao wanataka kuonyesha utiifu wao kwa Sankara wanayemtazama kama “Che Guevara wa Afrika", anasema.






SOURCE:Bbc Swahili




















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..