Mbowe asema migogoro ya Ukawa ni mambo madogo..

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Haikael MboweMwenyekiti wa Chadema, Freeman Haikael Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Dar/Mikoani. Wakati mzozo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukishika kasi katika maeneo mbalimbali nchini, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hayo ni mambo madogo na umoja bado uko imara.
Kauli ya Mbowe imekuja ikiwa ni siku moja baada ya kutokea mzozo wa wagombea udiwani Kata ya Mburahati kukunjana mashati wakati wa mkutano wa mgombea mwenza, Juma Duni Haji juzi.
Mbali na mzozo huo, sintofahamu iliibuka mwishoni mwa wiki iliyopita wakati viongozi wa juu wa NCCR-Mageuzi; Makamu Mwenyekiti, Leticia Mossore akiwa na Katibu Mkuu, Mosena Nyambabe na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu, kupingana na Mwenyekiti wao wa Taifa, James Mbatia, hasa katika kukiendeleza chama na mgawanyo wa majimbo.
Mbowe alisema umoja wao hautakufa, wanaosubiri ufe watasubiri san“Kumekuwa na kauli na maneno yanayosambazwa kwenye mitandao kuwa umoja huo unalegalega, ninawaambia ushirika wetu uko imara, migogoro iliyopo ni changamoto ndogondogo tu ambazo haziwezi kuathiri umoja wetu,” alisema Mbowe.
Hata hivyo, kauli ya Mbowe inakinzana na hali halisi kwani Jimbo la Geita na mengine yamekumbwa na migogoro ikiwamo kata ya Kalangalala mkoani Geita ambayo ina wagombea wawili wa vyama vya Chadema na CUF ambavyo ni miongoni mwa vinavyounda Ukawa.Maeneo mengine yenye migogoro ni katika Jimbo la Kigamboni, Kata ya Vijibweni yenye wagombea wawili.
Kaimu Katibu wa Chadema Kigamboni, Raymond Magese, alithibitisha kuwapo kwa mgogoro huo kati ya Isaya Charles (Chadema) na Selemani Mbogo wa Cuf.
Mgogoro mwingine Mkoa wa Morogoro, mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kilosa, Abeid Mlapakolo (CUF), alisema pamoja na kuwa na makubaliano ya kuachiana majimbo, mgombea wa Chadema Rajabu Msabaha bado anaendelea na kampeni katika Kata mbili za Jimbo hilo, kinyume na makubaliano ya Ukawa.
Katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Salama Omary (CUF), amelalamikia rafu za Chadema kumsimamisha mgombea wao licha ya Jimbo hilo kupewa CUF kwa mujibu wa Ukawa.
Mkoani Kilimanjaro katika Jimbo la Vunjo, wagombea udiwani 16 kutoka Chadema, wametangaza kutomuunga mkono mgombea ubunge wa Vunjo kupitia NCCR-Mageuzi, ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.
Hali hiyo imetokea baada ya vyama hivyo kushindwa kuelewana katika makubaliano ya kusimamisha baada ya Chadema na NCCR-Mageuzi kusimamisha wagombea wao wa udiwani kwenye kata zote 16 za jimbo hilo.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Mossore alilalamikia chama chake kuachiwa majimbo 12 ikilinganishwa na 67 mwaka 2010 akisema Ukawa imewarudisha nyuma katika kupata wabunge.



SOURCE:Mwananchi














Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..