Vyombo vya habari nchini vyatakiwa kuzingatia haki na usawa...
Vyombo vya habari nchini vimetakiwa viepuke kuwa chanzo cha chuki na mifarakano inayosababisha uvunjifu wa amani na mauaji, hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa vyombo vya habari nchini - MOAT Dr Reginald mengi ametoa tahadhari hiyo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kulinda na kudumisha amani, ulioandaliwa kwa pamoja na Sekretarieti ya Jumuia ya Afrika Mashariki na Asasi ya Trinity Group East Africa, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Richard Owora na Mwakilishi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya wamesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuepuka kuchochea uvunjifu wa amani.
Akizungumzia uzoefu wake Mwanahabari na Mwanaharakati kutoka Rwanda bw. Tom Nahiro amesema mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda yanaweza kutokea katika nchi nyingine iwapo waandishi wa habari hawatajiepusha na lugha za uchochezi wa chuki.
Wakati wa mkutano huo wawakilishi wa viongozi wa dini Sheikh Hamisi Mattaka na Mchungaji Thomas Poda pia walivitaka vyombo vya habari kuzingatia maadili na kufanyakazi zao kwa manufaa ya jamii.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni