Hati za kukamatwa zatolewa dhidi ya wapinzani: wasi wasi mkubwa Burundi...
Askari polisi akipiga doria katika mitaa ya Bujumbura, mji mkuu wa Burundi, mwishoni mwa mwezi Julai.
Vyote hivyo vinatuhumiwa kuanzisha kundi la uasi nchini na kula njama za zajiribio la mapinduzi dhidi ya Pierre Nkurunziza lililotibuka Mei 13 mwaka 2015. Valentin Bagorikunda amesema hayo kulingana na ripoti ya kamati ya uchunguzi iliyoteuliwa na Ofisi ya mashtaka ili kuendesha uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi lililotibuka. Rfi ilipata kopi ya ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ilitaja majina ya wapinzani wakuu na wanaharakati muhimu wa mashirika ya kiraia, miongoni ni Jean Minani, kiongozi wa chama cha Frodebu-Nyakuri, ambaye aliwahi kuwa mara mbili Spika wa Bunge.
Jean Minani ametupilia mbali ripoti hiyo ya Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa akibaini kwamba hawajibiki katika kazi yake. “ Watu wanauawa hadharani, watu wakishuhudia, Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa hasemi lolote... Miili ya watu waliouawa inagunduliwa hapa na pale nchini, maiti zinaokotwa zikiwa zimefungwa kamba, baada ya kukamatwa na polisi, kila mtu anafahamu wanaotenda maovu hayo, lakini Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa hasemi lolote wala kukataza maovu hayo. Watu wanafanyiwa mateso ya aina mbalimbali hadi wanauawa, Mwendesha mashtaka hasemi lolote ”, amelaani Jean Minani.
Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha Frodebu-Nyakuri Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa anautuhumu upinzani kwa kila maovu yanayotendwa nchi Burundi. “ Hiyo inamaanisha kuwa Mwendesha mashtaka mkuu hafai kuwa Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa na amekua sasa mfuasi wa Pierre Nkurunziza. Kwa hiyo tunasema hakuna aliyeshinda vita dhidi ya raia. Kila siku raia ndio hupata ushindi ”, ameongeza Jean Minani.
Kwa upande wake Innocent Muhozi, hakuna serikali Burundi
Vyombo vya habari binafsi na viongozi wao - wenyewe - walikuwa bado hawajatajwa na hata hivyo mwendesha alivituhumu kuunga mkono mapinduzi ya kijeshi yaliotibuka.. Kwa upande wake Innocent Muhozi, kiongozi wa shirika linalochunguza taaluma ya uandishi wa habari nchini Burundi (OPB), na mkurugenzi wa redio na televisheni Renaissance amesema tangazo hilo la Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa nchini Burundi ni mwendelezo ulio dhahiri wa ukandamizaji wa vyombo vya habari.
" Huu ni muendelezo wa kisiasa ambao unaendelea tangu miaka kadhaa iliyopita, utawala ukijaribu kukandamiza uhuru wa raia na haki ya kiraia. Mashtaka au mauaji ya jinai, kila mtu ana wasiwasi nchini Burundi ambapo inaonekana kuwa hakuna serikali wala taasisi yoyote halali, unapoona hali inavyoendelea kila kukicha nchini humo; mauaji, mauaji ya wafungwa, mateso ... Maovu yote hayo yanatekelezwa na Idara zinazodaiwa kuwa ni za serikali. Kwa upande wetu hali mbaya zaidi yaweza kutokea...", amesema Innocent Muhozi.
SOURCE:RFI Kiswahili
Maoni
Chapisha Maoni