Wanahabari wa Al-Jazeera wasamehewa Misri...

Mohamed Fahmy na Baher Mohamed
Mohamed Fahmy na Baher Mohamed walikuwa wamefungwa miaka mitatu jela

Rais wa Misri amewapa msamaha wanahabari wawili kati ya watatu wa Al Jazeera TV waliohukumiwa kwa kupeperusha habari za uongo.
Msemaji wa rais amesema Mohammed Fahmy, raia wa Canada, na Baher Mohamed, raia wa Misri, wamo kwenye orodha ya wafungwa 100 watakaoachiliwa huru baadaye leo.
Vyombo vya habari vilisema mtu wa tatu kutoka kwenye kesi hiyo pia ataachiliwa huru.
Haijabainika bado iwapo mwanahabari huyo ni raia wa Australia Peter Greste, aliyetimuliwa kutoka taifa hilo Februari.
Watatu hao walihukumiwa vifungo vya miaka mitatu jela mwezi uliopita baada ya kesi yao kufanywa upya.
Viongozi wa mashtaka waliwatuhumu kushirikiana na kundi la Muslim Brotherhood lake Rais Mohammed Morsi baada yake kuondolewa mamlakani na wanajeshi 2013.
Kundi hilo lilipigwa marufuku baada ya wanajeshi kuchukua mamlaka.
Wanahabari hao wamekanusha mashtaka hayo na kusema walikuwa wanaripoti tu habari.
Wataalamu wa masuala ya kisheria walisema mashtaka dhidi yao hayakuwa na msingi na yalichochewa na siasa.
Miongoni mwa walioachiliwa ni watetezi wa haki za raia Yara Sallam na Sanaa Seif, waliohukumiwa miaka miwili jela 2014 kwa kushiriki “maandamano haramu” wakiitisha kuachiliwa kwa wafungwa na kufanyiwa mabadiliko kwa sheria kuhusu maandamano.
Peter Greste, aliyefurushwa kutoka taifa hilo Februari, alihukumiwa akiwa hayumo kortini.




SOURCE:Bbc Swahili














Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..