Mabasi ya Muro yafungiwa kutoa huduma..
Uamuzi huo umekuja baada ya kuwepo kwa mfululizo wa malalamiko juu ya huduma zisizoridhisha za mabasi hayo kutoka kwa wananchi.
Barua ya Sumatra kwa kampuni hiyo juu ya uamuzi huo inasema katika mojawapo ya safari zake, basi la kampuni hiyo likitoka Dar es Salaam kwenda Arusha, liliharibika eneo la Chalinze majira ya saa tatu asubuhi na hadi kufikia saa sita usiku halikuw alimetengemaa huku abiria wakikosa usafiri mbadala na huduma nyingine za kibinadamu.
“Sumatra ilipokea pia malalamiko ya kutoka kwa abiria juu ya mabasi ya kampuni yako yanayotoa huduma kwa mikoa ya Dar es Salaam –Arusha na Dar es Salaam –Mwanza kuharibika kwenye maeneo ya Ruvu darajani,Maili Moja na Chalinze kwa nyakati tofauti,” inasema sehemu ya barua hiyo.
“Sumatra imeona huo ni ukiukwaji wa Kanuni namba 21 na 22 ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji kwa magari ya abiria ya mwaka 2007 na kanuni namba 11(1)(b) ya viwango vya ubora na usalama ya mwaka 2008.”
Sumatra imeitaka kampuni hiyo kufanyia matengenezo mabasi yake na kukaguliwa na mkaguzi kutoka jeshi la polisi na kutibitisha yanakidhi viwango vya kiufundi na kiusalama.
SOURCE:Mwananchi
Maoni
Chapisha Maoni