Mgombea urais CCM ahidi kuhakikisha mikataba ya ajira kwa sekta isiyo rasmi inatolewa...



Serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk.John Pombe Magufuli iwapo wananchi watampa ridhaaya kuwa rais imejipanga kuhakikisha hakuna mtu atakayaetajirika kwa kuwadhulumu wanyonge au kukwepa kodi na pia kuhakikisha mikataba ya ajira kwa sekta isiyo rasmi inatolewa.

Kauli hii inayotolewa na mgombea urais wa chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli inashabihiana na kauli mbiu yake ya hapa ni kazi tu sambamba na maandiko matakatifu ya asiyefanya kazi na asile lengo likiwa ni kuondoa dhuluma kwa wananchi wa hali ya chini ili kila mtanzania anufaike kwa jasho lake na si kuzulumu wengine kwa njia ya ufisadi na wizi hususani wanyonge wasio na watetezi sambamba na kuangalia suala la mikataba ya ajira katika sekta isiyo rasmi.
Aidha Dr Mgufuli amewataka watanzania kutoshawishika na lugha za laghai zinazotolewa na baadhi ya wagombea na badala yake wawachuje kwa kuangalia utendaji na uadilifu wao ili kumpata kiongozi atakayezisimamia rasilimali na maliasili ya taifa kwa faida ya watanzania wote.
 
Katika kuhakikisha sera na matarajio yake kwa watanzania zinasikika na kuwafikia watanzania wa jamii zote wakiwemo walemavu baadhi ya mikutano ya Dr Magufuli imekuwa na wakalimani wa lugha za alama ili kuwawezesha baadhi ya walemavu wa usikivu wanaohudhuria mikutano hiyo waweze kuelewa kile anachokisema huku akiwaahidi wananchi wa eneo la mbarali kurejesha zaidi ya heka 1800 alizopewa mwekezaji kinyume na taratibu.
 
Akitokea mkoani Shinyanga Dr Magufuli hii leo ameendelea na mikutano ya kampeni na kufanya mikutano midogo minane alikokuwa akisimamishwa njiani na wananchi kabla ya kufanya mikutano mikubwa minne katika maeneo ya Mbarali mkoani Mbeya, na kisha Ilembula na Makambako mkoani Njombe pia mafinga mkoani Iringa ambako anatarajiwa kuendelea na mikutano ya kampeni mkoani humo kabla ya kwenda mkoani Dodoma.







SOURCE:ITV





















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..