Utafiti wa taasisi ya TADIP Juu ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015..


TADIP ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiliwa mwaka 2006, miongoni mwa shughuli kuu za taasisi hiyo ni utafiiti na ushawishi wa sera na sheria nchini Tanzania.Tangu kuanzishwa kwake kimekuwa ikileta chachu katika maendeleo ya Tanzania.

Kupitia taasisi hiyo leo Sept 25 ilikutana na waandishi wa habari kuelezea tafiti zilizofanyika katika chaguzi hizi zinazoendelea 2015, kwa mujibu wa mkurugenzi wa bodi ya TADIP George Shembusho..Wananchi waliulizwa ni mgombea yupi wangemchagua kuwa rais ikiwa uchaguzi ungefanyika siku ambayo taarifa za utafiti huu zilizopokuwa zinakusanywa (wiki tatu za mwanzo, Septemba).Asilimia 54.5% ya washiriki walijibu kwamba wangemchagua Edward Lowassa, asilimia 40% wangemchagua Dkt. John Pombe Magufuli huku asilimia 2% walisema wangemchagua Anna Mghwira’ -George Shembusho

.

Wengine ni Hashimu Rungwe (0.4%) na Chief Yemba (0.1%) huku 3% wakiwa wamesema hawajui wangemchagua nani.Edward Lowassa anaungwa mkono zaidi mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Dar huku Dkt. John Magufuli akikubalika zaidi katika mikoa ya Dodoma na Morogoro kama inavyoonekana kwenye graph nambari 6′George Shembusho

Kukubalika



.

‘Kwa upande wa makundi ya umri, Edward Lowassa anaonekana kuungwa mkono zaidi na vijana pamoja na watu wenye umri wa kati (Miaka 18- 47), watu wazma wenye umri juu ya miaka 47 wanamuunga mkono zaidi Dr. John Magufuli’ – -George Shembusho





SOURCE:Millardayo.com













Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..