Tanzania yaongoza duniani kutoa huduma za kifedha kwa simu..
Dar es Salaam. Tanzania ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma za pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa kutumia mawasiliano ya simu, kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB)
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inanukuu taarifa ya Benki ya Dunia kuwa Tanzania ni moja ya nchi zenye masoko makubwa zaidi duniani ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu.
Katika taarifa inaongeza kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiwango cha juu katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.
Kwa mujibu wa Mchumi Mkuu wa WB, Benki Kuu, Prof Kaushik Basu Kenya inaongoza kwa kutuma pesa kupitia mfumo wa M-Pesa katika eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa eneo la kujidai la nchi tajiri tu duniani.
“Tuko katikati ya mapinduzi makubwa ya teknolojia, ambayo athari zake bado ni ngumu sana hata kubashiri. Na hizi ni shughuli ambazo miaka michache iliyopita zilikuwa hata hazina jina, lakini sasa inteneti na teknolojia ya digitali inabadilisha maisha ya kijamii na kisiasa ya binadamu,” alisema Profesa Basu.
Katika Mkutano wa wakuu wa nchi uliozungumzia Hali ya Enzi za Digitali (Digital Age) uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) Basu alisema huu ni mfano kutoka Afrika ambao unaweza kuigwa na nchi zote duniani.
Mkutano huo ni sehemu ya majadiliano kuhusu Malengo ya Maendeleo Mapya (SDG’s) ambayo yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) ambayo muda wake wa utekekezaji wa miaka 15 umefikia mwisho mwaka huu.
Maoni
Chapisha Maoni