Mh.Magufuli ahidi kukuza pato la taifa ili serikali imudu kutoa huduma kwa jamii...



Wananchi waishio katika mikoa ya Kigoma na Kagera wameiomba serikali ya awamu ya tano itakayoingia madarakani kuimarisha miundo mbinu hasa ya reli kwa kuunganisha na nchi jirani pamoja na uwepo wa bandari bubu ili kusaidia kuinua pato la taifa pamoja na uchumi wa maeneo hayo ambayo yako nyuma kimaendeleo ukilinganisha na maeneo mengine ya nchi.

Wananchi hao wametoa wito huo katika mikutano ya kampeni ya kusaka urais kupitia chama cha mapinduzi CCM na kuongeza kuwa baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo kumebainika kuwepo na kiasi kikubwa cha maliasili yakiwemo madini na hivyo uwepo wa bandari ya nchi kavu pamoja na miundombinu ya reli kutasaidia kuchochea kukuwa kwa biasahara na hivyo kuinua vipato vyao na kuondoakana na umasikini.
 
Dr Magufuli ambaye amekuwa mkoani Kigoma akinadi sera za chama chake cha CCM na kuomba ridhaa ya watanzania kumpa kura ili aweze kuwa rais wa awamu ya tano ameanza kampeni zake mkoani Kagera ambapo akizungumza na wananchi wa eneo la Biharamulo amewahakikishia kuwatumikia watanzania kwa uaminifu na uadilifu na kuahidi kufanya jitihada za kukuza pato la taifa ili serikali imudu kutoa huduma za kutosha na za uhakika kwa jamii ya watanzania.
 
Akiwa wilayani Biharamulo mgombea huyo wa urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli amehani msiba wa aliyekuwa mwalimu wake mkuu wa shule ya msingi marehemu Corneli ambapo kumefanyika sala fupi kwa ajili ya kumuombea.




SOURCE:ITV













Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..