Wizara ya Afya Zanzibar Yakabidhiwa Pikipiki Tano kwa Ajili ya Wakuu wa Vitengo vya Mkono kwa Mkono Zanzibar...
Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto (Save The Children) Bi Mali lisson, akitowa maelezo kabla ya kukabidhi Pikipiki kwa Wakuu wa Kitengo cha Mkono kwa Mkono wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika Viwanja vya Wizara ya Afya Mnazi Mmoja.Zanzibar.
Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto,(Save The Children) Bi Mali Lisson, akimkabidhi Pikipiki Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo, kwa ajili ya Wakuu wa Kitengo cha Mkono kwa Mkono Zanzibar, jumla ya pikipiki tano zimetolewa kwa kitengo hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akitia saini baada ya makabidhiano ya Pikipiki zilizotolewa Msaadda na Shirika la Watoto la Save The Children) kwa ajili ya kuimarisha kiteno cha Huduma za Mkono kwa Mkono Zanzibar
Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo akitowa shukrani kwa Shirika la Kuhudumia Watoto (Save The Children) wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya Kitengo cha Mkono kwa Mkono Zanzibar.
Jumla ya Pikipiki tano zilizotolewa na Shirika la Watoto kwa ajili ya kutowa huduma kwa Wakuu wa Kituo cha Huduma cha Mkono kwa Mkono Zanzibar.
SOURCE:ZanziNews
Maoni
Chapisha Maoni