Mgombea urais wa CCM ahidi kushughulikia kero ya ukosefu wa mikataba kwa madereva...



Mitaa ya mji wa Kahama na viunga vyake imeshindwa kupitika kutokana na wingi wa watu waliojitokeza kumpokea mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM Dr John Pombe Magufuli ambaye ameahidi kushughulikia kero ya ukosefu wa mikataba ya kazi kwa madereva sambamba na kushughulikia kero ya watendaji kuishi katika halmashauri tofauti na wanakofanya kazi.

Dr Magufuli ambaye amepata mapokezi makubwa mno kutoka kwa wakazi wa mji wa Kahama na viunga vyake ameelezea namna serikali yake ilivyojipanga kutatua kero zinazowakabili watanzania wa jamii mbalimbali ambapo amesema katika serikali yake hakutakuwa na mtumishi wa serikali atakayekuwa anafanya kazi katika halmashauri moja huku akiishi katika halmashauri nyingine kwa kuwa kero zote zitatatuliwa ili waweze kuishi maeneo wanayotoa huduma sambamba na kuwaahidi madereva kushughulikia tatizo la mikataba ya ajira.
 
Pia Dr Magufuli amewataka watanzania kutobweteka na matokeo ya tafiti mbalimbali zilizotolewa na kuonesha ushindi kwa Dr Magufuli na badala yake akawataka wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura jumapili ya October 25 ya mwaka huu ili kumpa ushindi wa kishindo.
 
Dr Magufuli ameendelea na ziara yake ya kusaka kura kutoka kwa wananchi baada ya mapumziko ya siku moja kupisha sikukuu ya Idd el haji akitokea mkoani Geita na kuingia mkoani Shinyanga ambapo hii leo pekee amefanya mikutano mikubwa ya hadhara ipatayo mitano achana na mingine takribani minane ya njiani alikokuwa akisimamishwa na wananchi katika maeneo alikokuwa akipita. Jumamosi ya sept 26 Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na kampeni zake mjini Shinyanga.





SOURCE:ITV













Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..