Baba mtakatifu Francis aanza ziara Cuba na Marekani...
Atashiriki katika ibada kubwa ya Jumapili kwenye uwanja wa Revolutionary Square kabla ya kufanya mazungumzo na rais Castro.
Baba mtakatifu Francis akipunga mkono akiwa tayari kuondoka Rome
Baba mtakatifu Fransis ameondoka Rome kwa jili ya ziara ya siku kumi nchini Cuba na Marekani nchini hizo mbili zilizokuwa mahasimu wakubwa ambazo hivi karibuni zimefikia makubaliano .
Rais wa Cuba Raul Castro atasalimiana na baba Mtakatifu Fransis wakati akiwasili Havana kwenye uwanja wa kimataifa wa Jose Marti Jumamosi mchana.
Atashiriki katika ibada kubwa ya Jumapili kwenye uwanja wa Revolutionary Square kabla ya kufanya mazungumzo na rais Castro.
Kiongozi huyo wa Cuba amefurahishwa sana na baba mtakatifu mwenye asili ya Argentina .
Baba mtakatifu pia atatembelea miji ya Hoguin na Sntiago wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Cuba akipanga kufanya ibada na wakatoliki kwenye miji hiyo kabla ya kuondoka kuelekea Washington.
Baba mtakatifu na maafisa wa Vatican waliwezesha miezi kadhaa ya mazunguzo ya faragha baina ya Havanna na Washington mwaka 2014 ambayo yalikamilika huku kukiwa na tangazo la kihistoria mwezi Desemba kutoka kwa Castroa na rais Barack Obama kwamba nchi hizo mbili zimekubaliana kurejesha mahusiano ya kidiplomasia.
SOURCE:VOA
Maoni
Chapisha Maoni