Mamia ya mahujaji wafariki katika mkanyagano Makka...



Watu wasiopungua 717 wamekufa, huku wengine 816 wamejeruhiwa leo jirani na mji mtakatifu wa Makka walikokwenda kuhiji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya nguzo muhimu katika Imani ya dini ya Kiislamu, maofisa Saudi Arabia wathibitisha.
Kwa mujibu wa Baraza la Taasisi na Jumuiya za Kiiislam nchini, kati ya mahujaji 2,000,000 waliokwenda Saudi Arabia mwaka huu, 1,500 wanatoka Tanzania.
 Japokuwa Msemaji wa Baraza hilo, Shekhe Rajabu Katimba amesema hakuna vifo vilivyokwisharipotiwa hadi sasa toka Makka, taarifa zisizo rasmi kutoka huko zinasema Mtanzania mmoja amekufa na mwingine amejeruhiwa baada ya kutokea mkanyagano.
  Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, katika maafa hayo, mahujaji wengine wasiopungua 816 wamejeruhiwa katika eneo la Mina. Vifo hivyo vimetokea ikiwa ni siku chache kupita baada ya kutokea jail nyingine ambapo winchi lilianguka na kuua watu 109 katika msikiti ambapo kulikuwa kukifanyika ibada ikiwa ni maandalizi ya kuelekea sikukuu ya leo.
 Haya ni maafa makubwa zaidi kutokea katika sikukuu ya Eid Al Hajj baada ya kupita takribani miaka 25. Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Wizara ya Usalama wa Raia nchini Saudi Arabia, maafa hayo yametokea kati ya saa sita (majira ya Afrika Mashariki) katika makutano ya mitaa namba 204 na 223 wakati mahujaji hao wakipanda ngazi kuelekea jengo la ghorofa tano ambalo limeuzunguka mnara, maarufu kwa jina la Jamarat Bridge. “Tukio hilo limetokea baada ya mahujaji kuongezeka ghafla wakielekea kwenye mnara,” taarifa ya wizara iliongeza.




SOURCE:Mwananchi




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..