Hali ya ugonjwa wa Kipindupindu DSM bado si shwari wagonjwa wanaongezeka siku hadi siku..
Hali ya ugonjwa wa Kipindupindu jijini Dar es Salaam bado si shwari ambapo katika kambi ya Mburahati idadi ya wagonjwa bado inazidi kuongezeka siku hadi siku licha ya elimu inayotolewa juu ya ugonjwa huo.
Afisa muuguzi wa kambi hiyo Bi Amina Mbweso amesema idadi ya wagonjwa inaongezeka na kupungua kila siku na hakuna siku ambayo hawapokei wagonjwa wa Kipindupindu usiku na mchana na kuongeza kuwa kwa sasa wana wagonjwa 25 ambao bado wanaendelea kupatiwa huduma ya matibabu.
ITV imetembelea kambi hiyo na kuzungumza na baadhi ya wagonjwa ambao bado wanaendelea na matibabu ambao wameelezea namna na mazingira waliopata ugonjwa huo.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni