Kili Stars kuanzia kwa Wasomali..



Dar es Salaam. Timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) itaanza harakati za kusaka ubingwa wa mashindano ya Chalenji kwa kuikabili Somalia katika mchezo wao wa ufunguzi Novemba 22 nchini Ethiopia.
Ratiba iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholaus Musonye ilionyesha kuwa Stars ambayo iko Kundi A itacheza mchezo wake wa kwanza mjini Addis Ababa.
Mchezo wa pili kwa Stars utakuwa Novemba 24 dhidi ya Amavubi ya Rwanda, uliopangwa kufanyika kwenye mji wa Awassa na kisha kucheza mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya wenyeji Ethiopia, Novemba 28.
Zanzibar Heroes wataanza kampeni ya kusaka ubingwa Novemba 21 wakiikabili Burundi katika mchezo wa ufunguzi wa kundi lao utakaopigwa mjini Addis Ababa.
Mechi ya pili kwa Zanzibar itakuwa dhidi ya Uganda Cranes, Novemba 24 na kuivaa Kenya siku tatu.
Robo fainali ya mashindano hiyo itachezwa Novemba 30 na Desemba Mosi na timu zitakazoshinda zitatinga nusu fainali itakayochezwa Desemba 3.
Timu nyingine zinazoshiriki mashindano hayo ni Sudan, Sudan Kusini, Djibouti na Malawi zilizoko Kundi C.
Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki aliwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuishangilia Jumamosi Taifa Stars ili ifanye vizuri kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia.
“Tunatarajia wakazi wa mji huu, na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kuishangilia Stars, Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli amethibitisha kuwapo uwanjani kuwashangilia vijana wetu na amethibitisha, labda yatokee majukumu mengine ya kitaifa.
Alisema pia wamemwomba Rais mstaafu Jakaya Kikwete iwapo atapata nafasi naye ahudhurie mchezo huo kwa lengo la kuhamasisha zaidi wachezaji.





SOURCE:Mwananchi





































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..