Zanzibar hali si nzuri baada ya bei za vyakula na vitoweo kupanda bei kwa asilimia kubwa...
Mgogoro wa kisiasa unaondelea kisiwani Zanzibar umeanza kuleta madhara yake baada ya bei za vyakula muhimu na vitoweo kupanda bei kwa asilimia kubwa na kuwaweka wazanziabri katika wakati mgumu.
Uchunguzi wa ITV umeonyesha bei za vyakula muhimu kama nyama ya Ng’ombe na Mbuzi kupanda kwa kilo moja kufika hadi 12,000 kutoka 800, huku bei za viazi vikiuzwa kilo 2000 badala ya 800, vitunguu, karoti na matunda mengine yakipanda bei mara mbili na bei za kawaida nayo yakizidi kuwapa makali ya maisha wananchi wa Zanzibar huku bei za samaki nazo zikiendelea kuwa tishio ambapo samaki moja mkubwa alikuwa akiuzwa16,500 badala ya 6,500.
Wakiongea na ITV baadhi ya wafanyabishara wa vyakula na kitoweo wakiongea na ITV wamemsema hali hiyo inatokana kwa hivi sasa hakuna chakula cha aina yeyote kinachoingia Zanzibar kutoka bara ambapo ndipo soko kubwa la mahitaji ya Zanzibar.
Naye moja wa mwananchi ambaye alikuwa akitafuta mahitaji yake katika soko kuu la Zanzibar Abubakar Pandu amesema wanaumia na hali hiyo hivyo njia pekee ni wahusika wamalize na wao wanalazimika kununua ili hawana sehemu nyengine ya kutafuta afueni.
Hata hivyo pamoja na ukali huo wa maisha mji wa Zanzibar umeendelea kuwa katika hali yake ya kawaida huku huduma za biashara na usafiri kwaakika mwendo wake wa kila siku ingawa kisiasa bado Zanzibar haijakuwa shwari na mvutano bado uanendelea kuwepo.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni