Lipumba aibukia ofisi za CUF, ataka JK aingilie kati suala za ZEC..

Mwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa IbrahimMwenyekiti wa zamani wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuiamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  (ZEC ) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa uliofanyika Zanzibar ili kuipusha nchi kuingia katika machafuko.
Jumatano iliyopita, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu akisema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi.
Akizungumza leo kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari tangu alipojiuzulu, Agosti 6, mwaka huu, Lipumba alisema  amelazimika kutoa ushauri baada ya kuona hatari iliyo mbele kama wananchi wa Zanzibar  watanyang’anywa haki yao.
 “Ijumaa ijayo Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania, Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo yaliyopo yanamtosha, ” alisema.
Lipumba ambaye alipokelewa na wafuasi zaidi ya 100 kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, alisema Kikwete ahakikishe kabla hajamaliza muda wake wanaiamuru ZEC kuendelea kutangaza matokeo na kuwatangaza washindi wa uchaguzi huo.






SOURCE:Mwananchi


































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..