Theluji mlima Kilimanjaro imepungua kwa asilimia 85 na inakadiriwa kumalizika ifikapo mwaka 2060...
Theluji katika mlima Kilimanjaro imepungua kwa asilimia 85 na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2060 itakuwa imemalizika kabisa kutokana na uharibifu mkubwa wa misitu katika hifadhi ya taifa ya mlima huo (kinapa) na mabadiliko ya tabia nchi.
Mhifadhi mkuu wa Kinapa Bw Erastus Lufungulo amesema, utafiti uliofanywa na wataalam wa ndani na nje ya nchi umeonyesha kuwa kupungua kwa theluji hiyo imesababisha ongezeko la joto katika bahari ya Hindi.
Hata hivyo Bw Lufungulo amesema, juhudi mbalimbali zimeanza kuchukuliwa na hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya doria za mara kwa mara katika eneo la msitu ili kuzuia watu wasikate miti na kupunguza matukio ya moto.
Mhifadhi wa utalii wa Kinapa Bi Eva Mallya amesema, ingawa hali hiyo haikuathiri sana utalii lakini idadi ya watalii imepungua kwa asilimia 3.4 kutoka watani 57.756 kwa miaka kumi iliyopita kila mwaka hadi watalii 51,256 kati ya mwaka 2013 hadi sasa.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni