Wizara ya afya imepiga marufuku migodi ya madini ya chumvi nchini iliyokiuka sheria.



Wizara ya afya na ustawi wa jamii imetishia kuifunga migodi yote nchini inayochimbwa madini ya chumvi na badala yake imepiga marufuku usafirishaji wa madini ya chumvi isiyokuwa na madini joto unaofanywa na wafanyabiashara wanaosafirisha kwa visingizio vya kupeleka kwenye viwanda vya utengenezaji wa ngozi, badala yake wamekuwa wakiisafirisha kwenye masoko ya ndani na nchi jirani na kuuzwa kiholela bila ya kujali madhara yatokanayo na chumvi hiyo isiyokuwa na madini joto.

Licha yawizara kutoa elimu ya matumizi ya madini joto ili kuepusha madhara 104 yatokanayo namatumizi ya kibindamu ya  chumvi hiyo, na sasa mkurugenzi msaidizi wa huduma na lishe Dr Vincent Assey amekutana na baadhi ya wachimbaji katika mgodi wa madini hayo ya chumvi hiyo inayochimbwa katika msimu wa kiangazi toka ziwa Gidewar kata ya Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara na kutoa  marufuku hiyo baada ya kubaini wachimbaji hao hawazingatii elimu waliyofundishwa ya matumizi ya madini joto (IODINE) kabla ya kuuza.
 
Katika ziara hiyo iliyowakutanisha wachimbaji wachache na wataalam hao wa afya wamejaribu kuwakumbusha kwa kutoa elimu ya papo kwa papo juu ya kuepukana na madhara 104 yanayosababishwa na matumizi ya chumvi hiyo ambayo hapa nchini zaidi ya wananchi million 5 wanasumbuliwa na ugonjwa wa tezi shingo (GOITRE) ambayo huanza kabla ya utungwaji wa mimba, matatizo mengine ni kudumaa kwamwili, kuharibika kwa mimba na usahaulifu.
 
Hata hivyo baadhi ya wachimbaji katika mgodi huo wa Gendabi uliopo ukanda wa bonde la ufa wamesema marufuku hiyo huenda ikawaathiri kiuchumi hasa katika msimu huu ambao soko lake limeshuka kutokana na msimu wa mvua za vuli, huku kauli ya mjumbe wa bodi ya taifa ya udhibiti wa madini joto Dr Louis Mmbando akisisitiza sheria ifuatwe bila ya shuruti.








SOURCE:ITV




























































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..