STARS YASHINDWA KUPATA USHINDI NYUMBANI
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza.
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeeshindwa kuchomoza na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na timu ya taifa ya Algferia kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi kwa ajili ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi.
Elius Maguli alianza kuifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 43 kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi. Goli hilo likaipeleka Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Algeria walisawazisha goli dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza mfungaji akiwa ni Slimani Islam bao ambalo limefungwa kutokana na uzembe wa walinzi wa Stars.
Dakika za mwanzo za kipindi cha pili Stara ilicheza mpira wa kasi na kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya …lililofungwa na Mwana Samatta baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Algeria kisha kufunga goli kwa ustadi wa hali ya juu.
Muda mfupi baada ya Stars kupata goli la pili kocha alifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Elius Maguli na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Muthir Yahya.
Dakika ya 74 kipindi cha pili, Slimani Islam aliisawazishia Aligeria goli lililotokana na kutoelewana kwa safu ya ulinzi ya Stars na kutoa mwanya kwa Slimani kuisawazishia timu yake.
Kikosi cha Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Elius Maguli na Farid Musa.
Wlioanzia kwenye benchi: Ailishi Manula (GK) Salim Mbonde, Mohamed Hussein, Simon Msuva, John Bocco, Mrisho Ngassa na Malimi Busungu.
SOURCE:Shaffihdauda.com
Maoni
Chapisha Maoni