TFDA yakamata kiwanda bubu cha kutengenezea chumvi Tabata Dar es Salaam...
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA kanda ya mashariki imekamata kiwanda bubu cha kutengeneza chumvi ikitahadhalisha watanania kutotumia chumvi yake iliyokwisha sambazwa nchini kote kwa sababu za uwezekano wa kuwa na viambata vyenye sumu na kuhatarisha afya zao.
Akiongea katika tukio hilo meneja wa tfda kanda ya mashariki bw. Emanuel alfonsi amesema kubainika kwa kiwanda hicho kilichokutwa kwenye makazi ya watu eneo la tabata jijini dar es salaam kunafuatia taarifa za raia wema ambao walianza kutilia shaka mazingira ya uzalishaji wa bidhaa zake na kuamua kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kumfikisha mmiliki wake katika vyombo vya sheria.
ambaye pamoja na kueleza kuwasilisha sampuli za bidhaa hiyo kwa mkemia mkuu ameelezea bidhaa hizo zenye alama ya mfaume salt au m.salt zimesambazwa katika mikoa ya kusini huku akiomba mamlaka za udhibiti na vyombo vya dola kuzuia matumizi yake hadi taarifa itakapo tolewa vinginevyo huku mmili wake bw. Mfaume rajabu akikiri kuendesha biashara hiyo kinyemela kwa kile alichokielezea kuwa ni kutojua kama kuna taratibu za kisheria anatakiwa kuziafuata.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni