Viongozi wa UKAWA kutoa tamko zito wiki hii juu ya uchaguzi wa Zanzibar...


Viongozi wakuu wanaounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA wamekutana jijini Dar es Salaam na kufanya kikao kizito ambapo wanatarajia kutoa msimamo wao kuhusu Zanzibar mapema wiki hii.


Mvutano wa kisiasa visiwani Zanzibar umemfikisha katibu mkuu wa CUF Malim Seif Sharifu Hamadi kwa aliyekuwa akigombea nafasi ya urais wa Tanzania Mh Edward Lowassa na kupokelewa na maafisa wa ngazi ya juu wa umoja huo.
 
Baada ya kikao kizito kilichodumu kwa dakika 30 kati ya viongozi wa umoja huo na katibu mkuu huyo wa Cuf ambaye pia ni makamo wa kwanza wa rais Zanzibar, Edwrad Lowassa akasema uamuzi mzito kuhusu Zanzibar ni jumapili wiki hii.
 
Kwa upande wake katibu mkuu wa CUF ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar Malim Seif, amesema hawako tayari kurudia uchaguzi wa Zanzibar.
 
Mvutano wa kisiasa visiwani Zanzibar umekuja baada ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salm Jecha kutangaza kuufuta uchaguzi huo siku chache baada ya kupigwa kura mapema Oct 25 mwaka huu kwa madai ya uwepo wa kasoro kadhaa katika uchaguzi huo.








SOURCE:ITV















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..