Maombolezo na hali ya hatari Ufaransa...
Shambulizi Paris
Kundi la wapiganaji la Islamic State limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya mashambulio ya mjini Paris Ijumaa usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Rais Hollande ameelezea mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa na IS ambao alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi.
Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume wanane waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo katika sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa.
Usalama waimarishwa Paris
Wakuu wanasema paspoti ya Syria ilionekana karibu na mwili moja.
Watu kama 80 walikufa katika tamasha la muziki wa roki - ambako washambuliaji waliwakabili mateka wao na kuwapiga risasi.
Maafisa wa polisi waimarisha doria za usalama Paris.
Hapo awali, watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi nyingi dhidi ya mikahawa iliyo karibu na kusababisha hasara kubwa.
Wengine waliripua mabomu karibu na uwanja wa michezo wa taifa, ambako Ufaransa ikicheza mechi ya kandanda na Ujerumani.
SOURCE:BBC
Maoni
Chapisha Maoni