Muundo mpya wa dawa ya malaria wazinduliwa nchini...

Badala vidonge  24 kwa dozi (pichani) wagonjwaBadala vidonge  24 kwa dozi (pichani) wagonjwa wa Malaria sasa watatumia vidonge 6 kwa dozi nzima. 



Dar es Salaam. Wagonjwa wa Malaria sasa watatumia vidonge 6  badala ya 24 kwa dozi nzima ikiwa ni sawa na asilimia 75 ya punguzo la mzigo wa vidonge, iwapo watatumia dawa aina ya coartem.
Dawa hiyo mpya imezinduliwa hivi karibuni jijini  ikiwa na muundo mpya  wenye lengo la kumpunguzia mgonjwa mzigo wa kumeza vidonge vingi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hiyo uliofanyika jijijni Dar es Salaam juzi , Mkuu wa Operesheni ya Malaria Afrika wa kampuni ya Novartes, Dk Nathan Mulure alisema kuwa muundo huo mpya una lengo la kumpunguzia mgonjwa mzigo wa kumeza vidonge vingi.
“Katika kuhakikisha mgonjwa anatimiza matakwa ya matibabu ya malaria muundo mpya umepunguza idadi ya vidonge.”, alisema Dk Mulure.
Kwa mujibu wa Dk. Mulure, ingawa ugonjwa wa Malaria unaweza kukingwa na kuponywa, lakini bado ni moja ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi katika nchi zinazoendelea.
Alisema kuwa kila mwaka watu zaidi ya milioni moja duniani hupoteza maisha kutokana na malaria , nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara zikiwa na vifo mara nane zaidi.
Alisema vifo vingi kati ya hivyo ni vifo vya watoto huku akibainisha kuwa Afrika pekee kila sekunde 60 (saa moja) mtoto hufariki kutokana na ugonjwa wa malaria .
Kwa upande wake mdau wa Malaria, Profesa Zulu Premji, alishauri kuwa ugonjwa wa malaria ni lazima kwanza uthibitishwe kwa vipimo sahihi vya kimaabara kabla ya kuanza matibabu.
  “Ni wakati wa kuondosha mtazamo wa kuwa kila homa ni malaria  kwa kupima kwanza kabla ya kutumia dawa,”alisema.
Alisema ingawa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria kwa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania vimepungua lakini bado kuna changamoto nyingi ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi katika kupambana na malaria.
Akizungumzia mapambanao dhidi ya ugonjwa wa malaria nchini, Profesa Premji alisema bado kuna changamoto nyingi zinazokwamisha ikiwa ni pamoja na utashi wa kisiasa pamoja na uwekezaji wa kutosha katika mapambano hayo.









SOURCE:Mwananchi



























































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..