Wachina mbaroni, wadaiwa kukutwa na pembe za faru..
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Thea Ntara amesema leo kuwa raia hao wamekamatwa baada ya kutiliwa shaka na maofisa wa Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato (TRA) katika Kituo cha Kasumulu kilichoko mpakani mwa Malawi.
Amesema maofisa hao walilitilia shaka gari lao aina ya Prado na kuamua kulikagua ndipo walipogundua kuwamo kwa pembe za faru, na kuchukua hatua ya kuwaita polisi.
Ntara amesema pasipoti za Wachina hao zilionyesha walitoka Msumbiji kupitia Malawi.
Wakati ukaguzi ukiendelea, Wachina watatu walitoroka kutoka Kasumulu lakini walikamatwa tena mjini Kyela wakiwa kwenye teksi waliokodi iwapeleke Tukuyu, wilayani Rungwe.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi alipoulizwa juu ya tukio hilo alithibitisha akiwa wilayani Kyela na kwamba angetoa taarifa kamili baada ya kurudi Mbeya
Hata hivyo RPC Msangi amesema upelelezi bado unaendelea.
Maoni
Chapisha Maoni