Dk.Maiga aagiza wakurugenzi wa mashirika kuacha kubuni miradi ya muda mfupi isiyo na tija..
Waziri wa mambo Nje Afrika Mashariki kikanda na kimataifa balozi Dk Agustino Maiga amewaagiza wakurugenzi wa mashirikia yaliyo chini ya wizara hiyo kuacha tabia ya kubuni miradi ya muda mfupi isiyo na tija kwa ajili ya kuwafurahisha viongozi au waonekane kuwa wanafanyakazi na badala yake wajenge miradi ya kudumu yenye maslahi kwa taifa na kizazi kijacho hata kama utekelezaji wake utachukua muda mrefu.
Balozi Agustino Maiga ametoa kauli hiyo jijini Arusha katika ziara ya kukagua miradi inayo tekelezwa na wizara ya mambo ya nje ambaye ilianzia katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC na ujenzi wa kituo cha kumbukumbu ya iliyokuwa mahakama ya kimbari ya Rwanda kinachojegwa jijini Arusha na kutoa agizo ilo kwa wakurugenzi wa mashihirika yaliyo chini ya wizara hiyo.
Mkurungenzi mtendaji wa kituo cha kimataifa cha AICC Elishiria Kaaya amesema AICC imewapokea maagizo ya waziri na tayari ilishaanza kutekeleza miradi imara na sasa kwa kushirikiana na wizara ya nishati na madini wanajenga kituo kikubwa cha madini kitakacho hifadhi na kuchakata madini ya vito bila kupeleka nchi za nje.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni