Zaidi ya shilingi Bilioni 500 zinahitajika kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa Nchini..
Tanzania inahitaji zaidi ya shilingi bilioni mia tano kwa ajili ya kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya, zahanati na Hospitali mbalimbali za serikali hapa nchini.
Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya dawa nchini ( MSD ) Laurean Rugambwa Bwana. Kunu amesema upatikanaji wa fedha hizo utaiwezesha Bohari hiyo kusambaza dawa nchini ili kuwawezesha wananchi kupata dawa kwa bei nafuu, ambapo katika mkoa wa Mwanza MSD imekamilisha maandalizi ya kufungua duka la dawa katika Hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure,ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dk.John Pombe Magufuli.
Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Dk.Faisal Issa amesema kuwa ongezeko la mapato ya serikali yatasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo.
Awali meneja wa MSD kanda ya ziwa Byekwaso Tabura pamoja na mganga mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dk.Onesmo Rwakendera wamesema kufunguliwa kwa duka hilo la dawa katika Hospitali hiyo kutatatua baadhi ya changamoto za upatikanaji wa dawa na hivyo kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Duka la dawa la MSD linatarajiwa kufunguliwa Januari nne mwaka 2016 ambapo duka hilo linataraji kuwahudumia wananchi wa mikoa sita ya kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza,Shinyanga, Mara, Simiyu, Geita na Kagera.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni